GET THE KCSE PREDICTION KISWAHILI P3 MARKING SCHEMES HERE

Bunyore

SEHEMU A

USHAIRI

  1. Lazima

               Monyara

Nakumbuka kwa dhiki Mto Monyara

Tuliochelea kukaribia kingo zake

Tukatulia kwanza; ukakamavu kujihamia

Kwa kunyenyekea  wingi wa yake maji

Yaliyojiendea utadhani yamesimama.

Ni katika mto huu

Ambapo samaki wakubwa tulivua

Maguo kuyatakasa japo kwa kunyemelea

Na walevi stadi wakachelea kuuvuka

Ulipofura na kupita kwa kiburi

Kwa kushiba maji yake

Yaliyofanya mawimbi madogo.

Ni hapa ambapo marehemu nyanya

Mkono alinishika na njia kuniongoza

Juu ya ulalalo wa miti

Vikapu vyetu hewani vikielea;

Mimi nikishika changu kwa mkono mmoja

Naye akikiachilia chake kujishikisha kichwani

Masafa baina yetu na mtambo

Uliokwenda kwa maji

Tuliyapunguza kwa kila hatua tulopiga.

Ni katika mto huu ambapo

Samaki tuliowavua tuliwapasua na kuwasafisha

Na hivyo kuuficha umaskini wetu

Ulotuzuia kununua mnofu wa bucha

Ni hapa ambapo wanawake walifika

Mawe ya kusagia kupata

Ni katika mto huu ambapo

Waumini walifika kutakaswa kwa ubatizo

Baada ya ulevi, uzinzi na kufuru nyinginezo.

Ni hapa ambapo ilisimuliwa kuwa

Hata wachawi walifika kufanya vitimbi vyao

Baada ya utawala wa jua kumezwa na nguvu za giza

Sasa Monyara nilioijua haipo tena

Zimebaki kingo zilizokaukiana

Kama uso wa mrembo aliyekosa mafuta

Siku ayami.

Mto huu ambapo pembeni mwake

Watoto walipashwa tohara

Maji yake yakishangilia, umekonda

Na mbavu zake nje kutoa

Na sasa vitoto vikembe vinazikanyaga

Vikijiendea zao kusaga mahindi

Juu mlimani

Katika mtambo wa Kizungu

Usioisha kulalamika

Nao wanawake hawaji tena

Kutafuta mawe ya kusagia wimbi

Imebaki njia ya walevi warejeao nyumbani

Nayo miti iliyosimama wima ukingoni

Iliisha kuanguka kwa kuleweshwa na pumzi za walevi

See also  A Silent Song And Other Stories KCSE Essay Questions and Answers-Series 1

Wasioisha kupita hapa.

  • Onyesha umuhimu wa Mto Monyara kwa wanakijiji.                        (alama 4)
  • Toa mifano ya mishata inavyojitokeza shairini.                                 (alama 2)
  • Eleza aina tatu za taswira zinazojitokeza katika shairi hili.               (alama 3)
  • Fafanua mtindo katika shairi hili.                                                       (alama 3)
  • Tambua nafsi neni ya shairi hili.                                                         (alama 1)
  • Jadili idhini ya kishairi katika shairi.                                                  (alama 3)
  • Andika ubeti wa pili katika lugha nathari                                           (alama 2)
  • Eleza toni ya shairi hili.                                                                      (alama 2)

SEHEMU YA B

Riwaya: Chozi la Heri  – Assumpta  Matei

Jibu swali la 2 au 3

2. “Wapo baadhi yetu ambao wizi unapotokea inasemekana wanashirikiana na wahalifu       wenyewe na baadaye wanagawana ngawira nao!”

a) 

  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili                                                           (alama 4)
  2. Jadili mtindo katika dondoo hili                                                               (alama 3)
  3. Eleza sifa za usemaji wa dondoo hili                                                       (alama 3)

b) Ufisadi unaojadiliwa katika dondoo  una madhara katika jamii ya Wahafidhina. Jadili.                                                                                                                                                  (alama 10)

3.

  1. Jadili mtindo kwenye dondoo hili.                                                                            (alama 8)

Jua linalochomoza halina ule wekundu wa jua la matlai ambao huleta haiba ya uzawa wa siku yenye matumaini. Naona wingu kubwa angani likitembea kwa kedi na madaha na kulifunika jua. Tukio hili linafuatwa na umeme, kisha mtutumo wa radi. Mawingu yaliyoshiba yakataka kutapika yanagooka, yanakaribiana, kupigana busu na kusababisha mwanguko wa matone mazito ya mvua; matone yanayoanguka kwenye ngozi laini za wanangu wakembe, Lime na Mwanaheri.  Nawatazama kwa imani lakini siwezi kuwasaidia.  Sina hata tambara duni la kuwafunikia.  Linalobaki ni kumshuru Mungu kuwa tungali hai.  Ubavuni mwangu amelala maskini mke wangu,Subira.  Sijui kama inahalisi kumwita mke wangu kwani huyu siye Subira wangu wa zamani.  Siye, siye, siye-e-e-e. Tazama uso wake ulivyovamiwa na majeraha, kikwi. Tazama  tambo lake lililoumbuka. Amevimba na kuvimbiana kama dongo la unga ngano baada ya kutiwa hamira.  Lakini yeye hana la hamira! Haya ni matokeo ya ubahaimu wa binadamu.  Kwa mbali namwona Ridhaa – mwamu hasa – akitafuna kitu fulani, nadhani ni mzizimwitu. Ridhaa, kweli Ridhaa kula mzizi! Daktari mzima! Mkurugenzi mzima wa Wakfu wa Matibabu nchini! Wanasema wajuao kuwa simba akikosa nyama hula nyasi. Msafiri kafiri ati! Amekosa la maama, hili la mbwa ataliamwa!

See also  Business Studies Topic By Topic Questions and Answers Form 1-4

b) “Huyu hapa ni Bwana Mwangemi na huyu hapa ni Bi Neema. Kama nilivyokujuza hapo awali, wamekuja kuchukukua kwenda kuishi nao kama mwana wao.”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.                                                              (alama 4)
  2. Banaisha mtindo katika dondoo.                                                              (alama 3)
  3. Toa sifa za msemaji wa dondoo hili.                                                        (alama 5)

SEHEMU YA C

Tamthilia: KigogoPauline Kea

Jibu swali  4 au 5

4.  Mwandishi wa tamthilia ya Kigogo amefanikiwa katika kutumia ishara ili kufanikisha maudhui.                                                                                                                     (alama 20) 

5. Mimi sili makombo kama kelbu! Nilishakunywa chai ya mke wangu nikaridhika.”

     (i) Eleza mkutadha wa dondoo hili.                                                                       (alama 4)

      (ii) Fafanua mtindo katika dondoo hili.                                                                 (alama 4)

      (iii) Jadili vile Wanasagomoyo wamefanywa kelbu kula makombo                        (alama 12)

SEHEMU D

Hadithi Fupi: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine – Chokocho Na D. Kayanda:

Jibu swali la 6 au 7

6.

i) Tathmini umuhimu wa Samueli Matandiko  Katika kuijenga hadithi, “Mtihani wa Maisha”                                                                                                                                              (alama 10)

ii) Fafanua shibe inavyomaliza Waafrika katika hadithi ya “Shibe Inatumaliza”.         (alama 10)

“Tulipokutana Tena” – Alifa Chokocho.

7a) ‘Jijini ni kuzuri. Kuna majumba makubwa, utapanda magari mazuri mazuri ya marafiki zetu, utakula vyakula vitamu na kupewa nguo za fahari. Utapelekwa shule kusoma na kwandika.’

  1. Jadili muktadha wa dondoo hili.                                                               (alama 4)
  2. Eleza taswira zinazojitokeza katika dondoo hili kwa kutoa mifano.       (alama 3)
  3.  Aliyoambiwa msemewa ni kinyume cha yaliyotokea.  Eleza.                (alama 8)

    b) Wahusika mbalimbali katika hadithi hii wanatumia njia nyingi kukabiliana na matatizo yanayowakumba. Zijadili.

                                                                                                                                    (alama 5)

SEHEMU YA E

Fasihi Simulizi

Malaika …..

See also  Predictions-Kassu Jet Kiswahili paper 2 with Marking Scheme

Nakupenda malaika x 2

Ningekuoa  mali we…..

Ningekuoa dada…..

Nashindwa na mali sina we…..

Ningekuoa malaika x 2

Pesa, zasumbua roho yangu x 2

Nami nifanyeje, kijana mwenzio

Nashindwa na mali sina we

Ningekuoa malaika x 2

  1. Tambua utungo huu.                                                                                 (alama 2)
  2. Toa sababu za jibu lako hapo juu                                                              (alama 2)
  3. Taja shughuli ya kijamii na shughuli ya kiuchumi inayodokezwa kwenye kipera hiki.

(alama 2)

  1.  Tambua nafsi neni na nafsi nenewa.                                                       (alama 2)
  2. Jadili vipi mwasilishji wa kipera hiki anaweza kuboresha wasilisho lake.(alama 6)
  3. Ni matatizo yapi yanayoweza kumkumbuka mkusanyaji wa kipera hiki nyanjani?    (alama 6)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *