Get The Marking Schemes Here

SEHEMU YA A INSHA                                                                                                                  ALAMA 20

Andika kisa kitakachomalizika kwa maneno:

….Hapo ndipo nilipong’amua kuwa watu wenye ukarimu na utu wapo licha ya kuwa ni nadra kupatikana. Mja huyo aliahidi kumtua mzigo uliomlemea.

SEHEMU YA ‘B’ UFAHAMU                                                  ALAMA 10

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.

Mtaa wa Kisumu Ndogo, viungani mwa jiji la Mombasa. Mgonjwa amekuwa mgonjwa malana.  Jamaa na marafiki walikuwa wameambiwa hospitali, “Mrejesheni nyumbani.” Kwa hiyo hamna matumaini tena ya kupata ahueni.  Huyu ni wa kukatika roho dakika yoyote kuanzia sasa.  Yu tayari kukutana na Muumba wake. Wamemrejesha kwenye kibanda chake kilichotalizwa udongo na kuezekwa makuti machakavu.   Amepotelea kwenye kitanda chake cha kamba.  Sharti utazame kwa makini ndipo ubaini kwamba palikuwa na mtu pale kitandani.  Kabakia sindano kwa ukondefu. Baadhi ya watu waliozika imani na huruma zao, watu wenye kejeli zilizopindukia, wanamwita mbu.

 Ukutani kumetandikwa fremu yenye picha yake alipokuwa bado na siha yake.  Alipokuwa anaikanyanga ardhi mpaka inatetemeka, wakati alipokuwa akisakatia kadanda timu ya Bandari FC kwenye Uwanja wa Manispaa na kote nchini.  Wakati alipoichezea timu ya taifa Harambee Stars wakati alipotamba jijini Mombasa.  Pale kila jicho jijini ilipomtumbulia yeye.  Wakati kila ulimi ukimsifia na kila sikio kupenda kusikia jina lake, Otii.

Jamaa zake si watu wa kusibiri mvua kunyesha ndipo waanze kutafuta pahala pa kununua mwavuli.  Wanaamini juu ya upangaji wa mikakati mapema.  Kwa hivyo, wamekutana jioni hiyo kando ya kitanda chake kupanga mikakati ya mazishi.

“Anzeni mapema kuchangisha fedha za kusafirisha maiti,” alisema mwenyekiti wa Chama cha Watu wa Nyumbani.  “Tutahitaji  kuchangisha fedha za kununua jeneza, mavazi ya kumvisha maiti pamoja na fedha za kukodisha magari ya kuchukua maiti na waombelezaji kutoka hapa Kisumu Ndogo, Mombasa, hadi Sidindi karibu na Kisumu Kubwa, Kisumu asilia.

See also  Mathematics Paper 1 Mocks-Kapsabet Boys

“Nizikeni hapa,” anasema muwele.  “Gharama zote hizo za kunipeleka Sidindi za nini?”

Kimya kinajiri.

“Unasikia anasema nini?” Anakumbusha mwanachama mmoja.

“Gharama hizo ni zetu si zake,” anajibu katibu wa chama.  “Yeye atuachie tupange mambo. Anahaha nini? Yeye si mbwa wa kutupwa barabarani au mwituni akishafariki bwana. Lazima tumzike nyumbani Sidindi.  Hatuwezi kukiuka mila na ada zetu kwa kumwachia mwenzetu kutupiliwa mbali kana kwamba hana kwao.”

“Nasema nizikeni hapa.”

“Unaskia vile anavyosema.”

“Kauli yake si  muhimu,”  mwenyekiti alisema.   “Katika mila na desturi zetu kauli ya marehemu si chochote, si lolote. Muhimu ni kwamba sharti mtu wa kwetu azikwe nyumbani.”

Wanapomtazama Otii wanaona anatokwa na chozi kwenye jicho moja lililokuwa halijafunikwa na shuka. Chozi linadondoka taratibu na kuteremikia kwenye shavu lake kavu kasha kumalizikia kwenye shuka.

Anapiga chafya na kukohoa mara kadhaa.

“Basi kila mtu  anajaribu awezavyo kukusanya fedha za kusafirisha maiti.  Sawa?”

“Sawa,” wanasema wote sawia.

Maswali.

1.   Thibitisha kuwa anayerejelewa katika makala haya alikuwa fukara.                        Alama 1

2.  Otii alikuwa Maarufu sana kabla ya kuwa mgonjwa.  Fafanua.                                             Alama 2

3. Eleza maana ya: “Jamaa zake si watu wa kusubiri mvua kunyesha ndipo waanze kutafuta pahala pa  

    kununua  mwavuli”.                                                                                                                  Alama 1

4. Chama cha watu wa nyumbani walifanya kinyume na matakwa ya Otii.  Eleza.                    Alama 1

5. Taja sifa zozote mbili zinazojitokeza za wahusika wanaopanga mikakati ya mazishi.           Alama 1

6. Andika na ueleze misemo yoyote miwili iliyotumika hatika hadithi hii.                                 Alama 2

7. Eleza maana ya msamiati. (i) Kilichotalizwa

                                               (ii) Muwele                                                                                          Alama 2         

SEHEMU YA ‘C’ SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA                                                           ALAMA 40

 1. Taja sauti zenye sifa zifuatazo
 2. Kikwamizo ghuna cha menoni
 • Irabu ya nyuma kati
 • Kiyeyusho cha midomo
See also  KIWAHILI P2 Questions and Answers

Alama  3

 • Kwa kutoa mifano tofautisha kati ya mizizi funge na mizizi huru.

Alama  2

 • Andika kwa ukubwa wingi:

Mji mkubwa umejengwa nyumba za kifahari.

Alama  2

 • Yakinisha sentensi ifuatayo;

Usipojikakamua kiume hutafaulu katika mitihani.

Alama  1

 • Tita ni la kuni ilhali ________________ ni kwa mizigo.                             Alama 1         
 • Weka nomino zifuatazo katika ngeli zake.                                                   Alama  2
 • Kijakazi
 • Petroli                                                                                                 
 • Kwa kutoa mfano, onyesha matumizi matatu ya kiakifishi:

Parandesi                                                                                                         Alama  3

 • Andiika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.

“Leo jioni tutamtembelea shangazi yako jijini”. Mama akamwambia

Alama  2

 • Changanua sentensi ifuatayo kwa mstari.

Sisi wawili tutatuzwa tuzo.                                                                             Alama  2

 1. Tunga sentensi katika wakati uliopita hali timilifu.                                      Alama  2
 1. Ainisha mofimu katika neno:

Apikaye                                                                                                           Alama  3

 1. Tunga sentensi ukitumia vivumishi vinavyotoa maana zifuatazo:               Alama  2
 • Kutobagua
 • Kutobakiza                                                                                         
 1. Unda nomino dhahania kutokana na vitenzi
 2. Safari
 • Lima                                                                                                    Alama 2
 • Tunga sentensi ukitumia kivumishi kisisitizi cha mbali kidogo ukitumia nomino ya ngeli ya I-ZI

Alama  2

 1. Tunga sentensi ukitumia kihusishi chochote cha wakati                              Alama 2
 1. Kamilisha jedwali.                                                                                        Alama 2
KutendaKutendeshaKutendeshea
Cheza    __________________________  __________________________
Lia    __________________________  __________________________
 1. Banisha vitenzi katika sentensi;

Babu yangu alikuwa akisafiri jana jioni

Alama  2

 1. Weka shadda kwenye maneno yafuatayo ili kubadilisha maana kwenye mabano.
 • Walakini    (dosari)
 • Barabara    (shwari)

Alama  2

 1. Unganisha sentensi ifuatayo ili kupata sentensi ambatano

Walimu hao walipewa uhamisho.

Walimu wengine hawakupewa

Alama  2

 • Andika katika wingi

    Ndizi hili langu limeoza.                                                                                   Alama1

SEHEMU YA ‘D’ ISUMUJAMII                                                                                       ALAMA 10

Soma kifungu kifuatacho  kisha ujibu maswali yanayofuata.

Niaje Wasee! Ma  likizo ndiyo hayo yameingia. Round hii tumefunga siku mob.  Mambo imebadilika.  Tukiwa ma holiday NI POA KUCHILL ili kuepukana na ball au magonjwa.

 1.  Tambua sajili ya makala uliyosoma.                                                              Alama2
 • Eleza sifa sita za sajili uliyotaja hapo juu.                                                      Alama 6
See also  KCSE Predictions Ushairi Questions And Answers- Shairi 1-5

Alama  2

 • Istilahi zifuatazo za isimujamii zina maana gani?
  • Lahaja
 • Uwililugha

SEHEMU YA E:  FASIHI SIMULIZI                                                                               ALAMA 10

 1. (a) Eleza maana ya:
 2. Ushairi simulizi                                                                       Alama1
 • Taja vipera viwili vya Ushairi simulizi                                   Alama2
 • Mbolezi huwa na umuhimu katika jamii.  Eleza umuhimu wake kwa hoja tatu. Alama 3
 • Fafanua aina zifuatazo za hadithi.                                                                              Alama  2
 • Mighani
 • Hurafa
 • Eleza aina mbili za hadhira.                                                                                       Alama  2

SEHEMU YA F:  USHAIRI                                                                                                ALAMA 10

Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali

Dunia yetu dunia, watu wanakufitini,

Dunia huna udhia, watu wanakulaani,

Dunia huna hatia, wabebeshwe kila zani,

Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia umenyamaza, umetua kwa makini

Dunia vitu, watu wanataka nini?

Dunia wanakucheza, binadamu maliani,

Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia utu akose, huvutia mdomoni.

Dunia ebu waase, hao watu mafatani,

Dunia chuki upuse, munipate afueni,

Dunia unaonewa, umetenda kosa gani?

Dunia pewa lawama, za uongo si yakini,

Dunia wanakusema, ni manjunju si raini,

Dunia huna hasama, waja ndio kisirani

Dunia unaonewa,umetenda kosa gani!

Dunia kuharibika, hayo amezusha nani?

Dunia watu humaka, hao wanaokuhini

Dunia umejazia, kila tunu ya thamani

Dunia unaonewa, umetenda kosa gani?

Maswali

 1. Taja sifa zozote mbili za binadamu kama zinavyojitokeza katika shairi.           Alama 2
 • Hii ni shairi ya aina gani kwa mujibu wa aina mbili kuu za mashairi.            Alama 1
 • Eleza umbo la ubeti wa tatu                                                                           Alama 4
 • Shairi hili linaweza kuwekwa katika bahari mbalimbali. Zitaje bahari mbili. Alama2
 • Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulifyotumika katika shairi.
 • Mafatani                                                                                         Alama 1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *