Get The Marking Schemes Here
SEHEMU YA A INSHA ALAMA 20
Andika kisa kitakachomalizika kwa maneno:
….Hapo ndipo nilipong’amua kuwa watu wenye ukarimu na utu wapo licha ya kuwa ni nadra kupatikana. Mja huyo aliahidi kumtua mzigo uliomlemea.
SEHEMU YA ‘B’ UFAHAMU ALAMA 10
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Mtaa wa Kisumu Ndogo, viungani mwa jiji la Mombasa. Mgonjwa amekuwa mgonjwa malana. Jamaa na marafiki walikuwa wameambiwa hospitali, “Mrejesheni nyumbani.” Kwa hiyo hamna matumaini tena ya kupata ahueni. Huyu ni wa kukatika roho dakika yoyote kuanzia sasa. Yu tayari kukutana na Muumba wake. Wamemrejesha kwenye kibanda chake kilichotalizwa udongo na kuezekwa makuti machakavu. Amepotelea kwenye kitanda chake cha kamba. Sharti utazame kwa makini ndipo ubaini kwamba palikuwa na mtu pale kitandani. Kabakia sindano kwa ukondefu. Baadhi ya watu waliozika imani na huruma zao, watu wenye kejeli zilizopindukia, wanamwita mbu.
Ukutani kumetandikwa fremu yenye picha yake alipokuwa bado na siha yake. Alipokuwa anaikanyanga ardhi mpaka inatetemeka, wakati alipokuwa akisakatia kadanda timu ya Bandari FC kwenye Uwanja wa Manispaa na kote nchini. Wakati alipoichezea timu ya taifa Harambee Stars wakati alipotamba jijini Mombasa. Pale kila jicho jijini ilipomtumbulia yeye. Wakati kila ulimi ukimsifia na kila sikio kupenda kusikia jina lake, Otii.
Jamaa zake si watu wa kusibiri mvua kunyesha ndipo waanze kutafuta pahala pa kununua mwavuli. Wanaamini juu ya upangaji wa mikakati mapema. Kwa hivyo, wamekutana jioni hiyo kando ya kitanda chake kupanga mikakati ya mazishi.
“Anzeni mapema kuchangisha fedha za kusafirisha maiti,” alisema mwenyekiti wa Chama cha Watu wa Nyumbani. “Tutahitaji kuchangisha fedha za kununua jeneza, mavazi ya kumvisha maiti pamoja na fedha za kukodisha magari ya kuchukua maiti na waombelezaji kutoka hapa Kisumu Ndogo, Mombasa, hadi Sidindi karibu na Kisumu Kubwa, Kisumu asilia.
“Nizikeni hapa,” anasema muwele. “Gharama zote hizo za kunipeleka Sidindi za nini?”
Kimya kinajiri.
“Unasikia anasema nini?” Anakumbusha mwanachama mmoja.
“Gharama hizo ni zetu si zake,” anajibu katibu wa chama. “Yeye atuachie tupange mambo. Anahaha nini? Yeye si mbwa wa kutupwa barabarani au mwituni akishafariki bwana. Lazima tumzike nyumbani Sidindi. Hatuwezi kukiuka mila na ada zetu kwa kumwachia mwenzetu kutupiliwa mbali kana kwamba hana kwao.”
“Nasema nizikeni hapa.”
“Unaskia vile anavyosema.”
“Kauli yake si muhimu,” mwenyekiti alisema. “Katika mila na desturi zetu kauli ya marehemu si chochote, si lolote. Muhimu ni kwamba sharti mtu wa kwetu azikwe nyumbani.”
Wanapomtazama Otii wanaona anatokwa na chozi kwenye jicho moja lililokuwa halijafunikwa na shuka. Chozi linadondoka taratibu na kuteremikia kwenye shavu lake kavu kasha kumalizikia kwenye shuka.
Anapiga chafya na kukohoa mara kadhaa.
“Basi kila mtu anajaribu awezavyo kukusanya fedha za kusafirisha maiti. Sawa?”
“Sawa,” wanasema wote sawia.
Maswali.
1. Thibitisha kuwa anayerejelewa katika makala haya alikuwa fukara. Alama 1
2. Otii alikuwa Maarufu sana kabla ya kuwa mgonjwa. Fafanua. Alama 2
3. Eleza maana ya: “Jamaa zake si watu wa kusubiri mvua kunyesha ndipo waanze kutafuta pahala pa
kununua mwavuli”. Alama 1
4. Chama cha watu wa nyumbani walifanya kinyume na matakwa ya Otii. Eleza. Alama 1
5. Taja sifa zozote mbili zinazojitokeza za wahusika wanaopanga mikakati ya mazishi. Alama 1
6. Andika na ueleze misemo yoyote miwili iliyotumika hatika hadithi hii. Alama 2
7. Eleza maana ya msamiati. (i) Kilichotalizwa
(ii) Muwele Alama 2
SEHEMU YA ‘C’ SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA ALAMA 40
- Taja sauti zenye sifa zifuatazo
- Kikwamizo ghuna cha menoni
- Irabu ya nyuma kati
- Kiyeyusho cha midomo
Alama 3
- Kwa kutoa mifano tofautisha kati ya mizizi funge na mizizi huru.
Alama 2
- Andika kwa ukubwa wingi:
Mji mkubwa umejengwa nyumba za kifahari.
Alama 2
- Yakinisha sentensi ifuatayo;
Usipojikakamua kiume hutafaulu katika mitihani.
Alama 1
- Tita ni la kuni ilhali ________________ ni kwa mizigo. Alama 1
- Weka nomino zifuatazo katika ngeli zake. Alama 2
- Kijakazi
- Petroli
- Kwa kutoa mfano, onyesha matumizi matatu ya kiakifishi:
Parandesi Alama 3
- Andiika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
“Leo jioni tutamtembelea shangazi yako jijini”. Mama akamwambia
Alama 2
- Changanua sentensi ifuatayo kwa mstari.
Sisi wawili tutatuzwa tuzo. Alama 2
- Tunga sentensi katika wakati uliopita hali timilifu. Alama 2
- Ainisha mofimu katika neno:
Apikaye Alama 3
- Tunga sentensi ukitumia vivumishi vinavyotoa maana zifuatazo: Alama 2
- Kutobagua
- Kutobakiza
- Unda nomino dhahania kutokana na vitenzi
- Safari
- Lima Alama 2
- Tunga sentensi ukitumia kivumishi kisisitizi cha mbali kidogo ukitumia nomino ya ngeli ya I-ZI
Alama 2
- Tunga sentensi ukitumia kihusishi chochote cha wakati Alama 2
- Kamilisha jedwali. Alama 2
Kutenda | Kutendesha | Kutendeshea |
Cheza | __________________________ | __________________________ |
Lia | __________________________ | __________________________ |
- Banisha vitenzi katika sentensi;
Babu yangu alikuwa akisafiri jana jioni
Alama 2
- Weka shadda kwenye maneno yafuatayo ili kubadilisha maana kwenye mabano.
- Walakini (dosari)
- Barabara (shwari)
Alama 2
- Unganisha sentensi ifuatayo ili kupata sentensi ambatano
Walimu hao walipewa uhamisho.
Walimu wengine hawakupewa
Alama 2
- Andika katika wingi
Ndizi hili langu limeoza. Alama1
SEHEMU YA ‘D’ ISUMUJAMII ALAMA 10
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Niaje Wasee! Ma likizo ndiyo hayo yameingia. Round hii tumefunga siku mob. Mambo imebadilika. Tukiwa ma holiday NI POA KUCHILL ili kuepukana na ball au magonjwa.
- Tambua sajili ya makala uliyosoma. Alama2
- Eleza sifa sita za sajili uliyotaja hapo juu. Alama 6
Alama 2
- Istilahi zifuatazo za isimujamii zina maana gani?
- Lahaja
- Uwililugha
SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI ALAMA 10
- (a) Eleza maana ya:
- Ushairi simulizi Alama1
- Taja vipera viwili vya Ushairi simulizi Alama2
- Mbolezi huwa na umuhimu katika jamii. Eleza umuhimu wake kwa hoja tatu. Alama 3
- Fafanua aina zifuatazo za hadithi. Alama 2
- Mighani
- Hurafa
- Eleza aina mbili za hadhira. Alama 2
SEHEMU YA F: USHAIRI ALAMA 10
Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali
Dunia yetu dunia, watu wanakufitini,
Dunia huna udhia, watu wanakulaani,
Dunia huna hatia, wabebeshwe kila zani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia umenyamaza, umetua kwa makini
Dunia vitu, watu wanataka nini?
Dunia wanakucheza, binadamu maliani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia utu akose, huvutia mdomoni.
Dunia ebu waase, hao watu mafatani,
Dunia chuki upuse, munipate afueni,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani?
Dunia pewa lawama, za uongo si yakini,
Dunia wanakusema, ni manjunju si raini,
Dunia huna hasama, waja ndio kisirani
Dunia unaonewa,umetenda kosa gani!
Dunia kuharibika, hayo amezusha nani?
Dunia watu humaka, hao wanaokuhini
Dunia umejazia, kila tunu ya thamani
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani?
Maswali
- Taja sifa zozote mbili za binadamu kama zinavyojitokeza katika shairi. Alama 2
- Hii ni shairi ya aina gani kwa mujibu wa aina mbili kuu za mashairi. Alama 1
- Eleza umbo la ubeti wa tatu Alama 4
- Shairi hili linaweza kuwekwa katika bahari mbalimbali. Zitaje bahari mbili. Alama2
- Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulifyotumika katika shairi.
- Mafatani Alama 1