Get Marking Schemes From Here

  1. INSHA – ALAMA 20

“Wewe ni mwalimu mkuu wa shule yako. Andika hotuba utakayoitoa siku ya wazazi shuleni mwako.”

UFAHAMU

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali uliyoulizwa.                                              (ala 15)

Mateso ya wanawakiwa ni suala la kijamii linalofaa kutazamwa kwa darubini kali. Hata hivyo wanoathirika zaidi ni watoto ambao bado wako katika umri unaohitaji kulelewa na kupewa mahitaji ya msingi kama mavazi, malazi, elimu na mengine anuwai. Hali ya kuachwa na wazazi imekuwa ikizikumba jamii tangu enzi  za mababu na kila  itokeapo, wanajamii huipokea kwa mitazamo tofautitofauti, hivyo kuwafanya wanawakiwa kuathirika sana.

            Baadhi ya jamii zina imani za kijadi pamwe na mila zilizochakaa zinazozifanya kuamini kuwa baadhi ya vifo hutokana na laana. Wengine  huchukulia kuwa mwendazake ameondolewa na ulogi. Imani kama hizi huifanya jamii kuwatia watoto waliochwa katika mkumbo ule ule, hivyo kuwaangalia kwa macho yasiyo ya kawaida. Hii husababisha dhana gande.  Hali hii husababisha kuwachukulia watoto kama wanaotoka katika kizazi kilicholaaniwa. Jamii basi hukosa kuwapa watoto hawa stahiki yao. Hata wanapojitahidi kuiwania nafasi yao, waliowazunguka  huwavunja mioyo. Jitihada zao huishia kuwa si chochote kwa kuwa jamii inawatazama kama waliolaaniwa.

            Punde baada ya mzazi mmoja au wote wawili waendapo wasikorudi, inatarajiwa kwamba aliyeachiwa  mtoto awe mzazi wake, mwanafamilia au jirani awajibike na kumtunza mwanamkiwa. Kunao kadha wa kadha wanaowajibika – nina wavulia kofia. Hata hivyo wengi hutelekeza jukumu hii walilopewa na Muumba. Si ajabu basi kuona kuwa idadi ya watoto wanaozurura mitaani  inazidi  kuongezeka kila uchao. Ukichunguza utakuta kuwa wengi wa watoto hawa ni waliopotelewa na wazazi  wao. Inakera zaidi kugundua kuwa baadhi ya watoto hawa wana mzazi mmoja. Kwamba mke au  mume wa mtu ameaga, au iwe kwamba mzazi mmoja alimza mtoto na kumwachia mwenzake mzigo wa ulezi, aliyeachiwa na jukumu la kumpa mwanawe mahitaji ya msingi. Machoni pa  jalali, kila anayeupuuza wajibu huu ana hukumu yake siku ya kiama!

            Ni haki ya kila mtoto kupata elimu. Katika katiba ya Kenya mathalan, elimu ya msingi, yaani kuanzia shule ya chekechea hadi kidato cha nne ni ya lazima. Tangu hapo hata hivyo, jamii zimekuwa zikiwanyima wanawakiwa wengi elimu. Kwamba kunao wachache wanaowaelimisha baadhi ya  wanawakiwa ni kweli. Hata hivyo, wengine hukosa hata wa kuwapeleka katika shule ya chekechea, hivyo  kuishia kutojua hata kuandika majina yao. Mfikirie mtu katika karne ya 21 asiyejua kusoma wala kuandika! Nani ajuaye,  huenda  huyo  mwanamkiwa asiyepelekwa shuleni ndiye angalikuwa profesa, daktari, mwalimu, rubani au msomi mtajika na mtaalamu wa uwanja muhimu katika  jamii!

See also  Free 2022 Dec KCSE Papers With Marking Schemes

            Kila mtoto ana haki ya kulelewa hadi kufikia utu uzima kabla ya kupewa majukumu mazito. Katika katiba ya Kenya, utu uzima, ulio umri wa kuanza kufanya kazi huanzia miaka 18. Wanaohakikisha watoto hawa wametimiza utu uzima kabla ya kufanyizwa gange ngumu wanafaa pongezi. Hata hivyo wanawakiwa wamekuwa wakitumiwa na wengi kama punda wa huduma. Wanaaila wengine huwachukua wanawakiwa kwa machozi mengi  wazazi wao waagapo na kuapa kuwahifadhi na kuwatunza wana wale wa ndugu zao, kumbe ni machozi ya simba kumlilia swara! Hata kabla ya mwili wa mzazi mhusika kuliwa  na viwavi, mateso kwa mtoto yule  huanza, akawa ndiye afanyaye kazi zote ngumu. Utakuta watoto wao wamekaa kama sultan bin jerehe huku mwanamkiwa yule akiwapikia, kuwafulia nguo, kudeki, karibu hata wa waoshe miili! Kazi kama  zile za shokoa huwa za sulubu na aghalabu husindikizwa kwa matusi yasiyoandikika.

            Baadhi ya waja walionyimwa huruma huwahadaa wanawakiwa na kuwapeleka ng’ambo wakitumia vyambo, kuwa wakifika kule watapata kazi  za kifahari. Maskini wale huishia kushikwa shokoa, wakawa watumwa katika nyumba za waajiri wao, bila namna ya kujinasua. Wengine huishia kutumiwa kama watumwa wa  ‘Kimapenzi’ katika madanguro, miili yao ikawa ya kuuziwa makahaba waroho wasiojali utu.  Kujinasua kule huwa sawa na  kujitahidi kuokoa ukuni uliokwishageuka jivu, maadamu wanawakiwa aghalabu  hukosa watu wenye mioyo ya huruma ya kuwashughulikia. Wengi huitumia methali ‘ mwana wa ndugu kirugu mjukuu mwanangwa’ kuwapuuzilia mbali wanawakiwa ambao hukimbiliwa tu wabinafsi hawa wanapofaidika wenyewe.

  1. Kipe kifungu hiki kichwa mwafaka.                                                              (ala.1)
  • Eleza dhana ya  ‘Mwanamkiwa.                                                                     (ala. 1)
  • Ni kategoria gani ya wanawakiwa inayosumbuka sana?                               (ala. 2)
  • Taja mambo mawili ambayo baadhi ya imani na mila za jadi huchukulia kuwa  chanzo cha uanaukiwa.                                                                                                 (ala.1)
  • Eleza kwa kifupi hali ya elimu ya wanawakiwa.                                           (ala.2)
  • Taja mateso mawili ambayo wanawakiwa wanaoahidiwa kulepekwa ng’ambo hukumbana nayo.                                                                                     (ala.2)
  • Eleza unafiki wa baadhi ya watu wa jamii ya wanawakiwa.                         (ala.3)
  • Eleza maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika makala.       (ala.3)
  • Inakela
  • Waja
  • Kujinasua

UFUPISHO

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali uliyoulizwa

Wanawake wanaoishi katika maeneo ya mashambani katika nchi zinazoendelea ni baadhi ya watu waliotopea na kubobea kwenye umaskini mkubwa na wanaoathiriwa  na matatizo kwa kiwango kikubwa ulimwenguni. Jumla ya idadi ya wanawake  hawa wanaoishi chini ya kiwango cha chini cha umaskini inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 600. Hii ni idadi kubwa hasa ikikumbukwa kuwa ni asilimia kubwa ya wanawake wanaoishi kwenye maeneo haya.

See also  Asumbi Girls Form 4 Midterm 2 Exams 2023 With Marking Schemes

            Ulimwengu umeshuhudia ongezeko la idadi ya watu au dadiwakazi; kuwako kwa matatizo ya kiuchumi ulimwenguni; mitafaruku na vita vya kikabila, majanga ya kiasilia kama mafuriko ya maji, ukame au milipuko ya volkeno katika maeneo yanayoathiriwa nayo. Sababu nyingine ni uharibifu na ushukaji wa hali ya kimazingira, mabadiliko ya desturi au thamani za kitamaduni; kusambaratika kwa familia au misingi ya familia; utengano na hasa wakati wa shida pamoja na uhamaji wa wanaume na kuwaachia jukumu kubwa. Aidha kuna kuongezeka kwa hali ya wanawake kuwa wazazi pekee na hivyo kuongeza idadi ya miji inayoongozwa na wanawake na kukosekana kwa mikakati bora au ifaayo ya kupambana na maisha.

            Wanawake wanaoishi mashambani wanaathrika vibaya sana. Kwanza, kama masikini wanaishi katika mazingira makali. Pili, kama wanawake wanakabiliana na mapendeleo ya kisera na kitamaduni ambayo yanaudharau na kuupuuza mchango wao katika maendeleo. Tatu, kama viongozi wa miji (hasa wale wanaolea na kuzitunza jamaa zao peke yao) wanalazimika kupambana na uongozi wa miji pamoja uzalishaji. Aghalabu hawapati usaidizi au auni yoyote katika majukumu kama haya: wanalazimika kupambana nayo peke yao. Katika hali zote tatu zilizotangulia, wanawake hawapati nafasi  zifaazo  kushiriki katika maamuzi ya masuala yanayowahusu. Masuala mengi yanaamuliwa na wanaume bila ya kuwahusisha.

            Licha ya dhiki yao kubwa, wanawake hawa wanachangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa njia tatu kuu. Mchango huu unaonekana  katika kiwango cha jamii na taifa, kiwango cha mji na kupitia kwa kizazi kijacho. Katika kiwango cha kijamii na kitaifa, wanawake hawa ni chanzo cha nguvukazi. Nguvukazi hii inatokana na wao wenyewe pamojo na kizazi chao. Pia ni msingi muhimu wa uwekaji  rasilmali na kuhifadhi; aghalabu wana uwezo bora wa kutunza chochote walicho nacho kuliko wanaume. Katika kiwango cha mji, wanawake wa mashambani  wanahakikisha kuwako kwa chakula, na njia za kukitayarisha chakula hicho. Katika kiwango cha vizazi, wanawake  hawa wanakuwa kiungo kikubwa kati ya kizazi kijacho na vizazi vya kesho. Hawa ndio wanaowatunza, kuwalea na kuwaelimisha watoto na kuhakikisha kuwa pana muungano kati ya vizazi vya jamii.

  1.  Ni sababu zipi zinazosababisha umaskini wa wanawake wa shambani? (Maneno 50 -55)
See also  PHYSICS Paper 1 Questions and Answers

Matayarisho

Jibu

  • Eleza jinsi wanawake wa mashambani wanavyoathirika vibaya( maneno 40 – 45)

Matayarisho

Jibu

Sarufi na matumizi ya lugha.                                                                          (ala. 40)

  1. Eleza sifa mbili za sauti|k|.                                                                   (ala.2)
  • Andika mfano mmoja wa neno lenye muundo ufuatao:                                  (ala.1)

                    IKII

  • Sentensi ambatano ni ipi?                                                                    (ala. 2)
  • Unda sentensi yenye muundo ufuatao.                                                            (ala.2)

W+V+T+E

  • Onyesha viwakilishi (w) katika sentensi ifuatayo na ueleze ni vya aina gani. (ala. 2)

Wote walipewa kile kizuri.

  • Yakinisha sentensi ifuatayo.                                                                            (ala. 1)

      Hakula akashiba.

  • Kanusha sentensi ifuatayo.                                                                               (ala.2)

Ningeenda kwake leo angenipa mawaidha.

  • Eleza dhana zinazojitokeza katika maneno yaliyopigiwa mstari.                    (ala.3)

a)Mtoto mwenyewe alianguka mle

  • Mtoto mwenye tabia nzuri ni Yule.
  1. Tunga sentensi kuonyesha vielezi vifuatavyo.                                                 (ala.3)
  2. Kielezi cha wakati
  • Kielezi cha mahali
  • Kielezi cha namna/jinsi
  • Andika katika msemo halisi.                                                                            (ala. 2)

Rafiki yetu alitujulisha kuwa tungeondoka siku iliyofuatia kuelekea Afrika kusini.

  • Unda nomino kutokana na maneneo yafuatayo.                                              (ala. 3)

Neno                                                      Nomino

  1. Fikiri                                           ____________
  2.  – la                                                                                
  3. kubwa
  4. Tunga sentensi moja moja kuonyesha aina zifuatazo za nomino.                   (ala. 2)
  5. Nomino kitenzi – jina
  1. Nomino dhahania
  • Onyesha vivumishi (v) kwa kupigia mstari na ueleze ni vya aina gani.          (ala.2)

Waziri wa kawi anaishi katika nyumba kubwa.

  • Tumia alama ya ritifaa katika sentensi kuonyesha matumizi mawili tofauti. (ala. 2)
  • Bainisha viambishii katika neno  lifuatalo.                                                      (ala.3)

Waliotutenga

  • Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ulizopewa.                                      (ala.6)

Kitenzi                          tendesha                      tendeshea

Piga                               ___________              ________

-la                                 ____________            __________

-nywa                            ___________              ___________

  • Mahali palipotayarishwa pamejaa wageni kutoka mbali. ( Anza kwa: wageni…) ( al.2)

IV ISIMU – JAMII

Mtu X :           wauza how much?

Mtu Y:            Hamsini kastoma.

Mtu X:            Kumbe ni expesive hivyo?

Mtu Y:            Nitakupunguzia. Toa arobaini.

Mtu X:            Haya. Nipatie change.

  1. Hii ni sajili gani?                                                                                (ala.1)
  • Eleza sifa tano  za sajili hii.                                                                (ala5)
  • Taja athari mbili hasi za lugha ya ‘Sheng’                                         (ala.2)
  • Kwa nini vijana hutumia lugha ya ‘Sheng’ Eleza sababu mbili.        (ala.2)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *