KCSE Predictions Ushairi Questions And Answers- Shairi 1-5
USHAIRI WA 6
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Wataalamu muwe macho, vuani moto muenge,
Muenge hicho ambacho, cha watu wenye mawenge,
Mawenge yenye kijicho, kiswahili wakivunge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
Sichafue kiswahili, barakala tuwapinge,
Apige kila hali, wasiguse tuwainge,
Tuwainge wende mbali, kiswahili tujijenge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
Sichafue yetu lugha, waharibu Wabanange,
Wabanange iwe nyagha, waiweke tengetenge,
Lugha kuitwa; ulugha, lafidhi watia denge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
Tuichange heshima, na ulugha tuupinge,
Tuhifadhi kwa salama, na kisingio unyonge,
Kelele za maamuna, si watu ni visinge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
Kasema sheikh Amri, kiswahili tukisenge,
Kistawi kinawiri, kitumike kwenye bunge,
Hii ni yetu fahari, lugha yetu tuichunge.
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
Kikipatwa na maradhi, kwa sindano tukidunge,
Kila jama kutidhi, kipatwe hapo tupunge,
Tukitia mfawadhi, kama kunde na kihenge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
MASWALI YA USHAIRI
(a) Ni mtindo gani aliotumia mshairi katika kutunga ubeti wa 1 na 2. (fafanua kwa kutoa mfano)
(alama 4)
(b) Mshairi ametoa mapendekezo kadha katika shairi kuhusu jinsi ya kuimarisha na kuhifadhi lugha ya kiswahili. Taja na ufafanue matano kati ya hayo. (alama 5)
(c) Mshairi anazungumza na akina nani? Anazungumzia nini? (alama 4)
(d) Mshairi ametumia tamathali mbalimbali kuwasilisha ujumbe wake. Taja mifano mitatu tofauti ya tamathali hizo. (alama 3)
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi. (alama 4)
- Muenge
- Barakala
- Mtawadhi
- Maamuma.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA SHAIRI LA 6
8.a) – Mtindo wa sabilia: mshororo wa mwisho (kibwagizo) imerudiwarudiwa
– Pindu: neno moja au sehemu yote ya ubeti wa kwanza hutumiwa kama ukwapi wa ubeti unaofuata
- Anapendekeza wataalamu wawe macho ili maweye walindwe
– Kizazi cha sasa wasiige wenye kutaka kugandamiza Kiswahili
– Barakala wapigwe vikali
– Ifanywe lugha murwa/ rasmi bungeni
– Sindano kipigwe kikipatwa na maradhi
- Anazungumza na kizazi cha kisasa ili waitunze, kuitukuza na kulinda Kiswahili
Anazungumza juu ya kule kuhifadhi lugha ya Kiswahili
- Takriri- Kibwagizo kinarudiwarudiwa kutilia mkazo
Tashihishi-mfano: “kipatwa na maradhi kipigwe sindano” (lugha-uhai)
Chuku-Uzuri wa lugha umeongezwa chumvi
- Muenge-Kujitayarisha/ kujihadhirisha
Barakala-Wanaoiga desturi ya kigeni
Mfawadhi-Jitihada
Maamuma-Watu waja
9. a) Kwa vyovyote vile kile anachoona ni chake na ni halali kwake ataitetea mpaka apate/ apewe
- SAKARANI – Sababu beti la Takhmisa na la Tarbia zimechanganywa kuitunga
-Ubeti wa kwanza ni wa aina ya takhmisa (mishororo mitano) na ubeti wa pili ni Tarbia
-Ubeti wa pili una mishororo minne na vina vya ndani ni tofauti
Mizani ni nane ukwapi na utao (16 kwenye mshororo)
Uhuru wa lugha k.m taidai badala- nitadai
- Yu tayari kufanya kila jambo hata ikiwa ni kwa ncha ya upanga ikiwa mlimani, baharini, yu tayari kufuatilia
- Msanii anawapa motisha wasanii wake wawe wakiishi wakijua haki zao ni lazima wapewe la sivyo waitetee kwa vyovyote vile
- Mwandishi anasema kuwa izingirwe na ilindwe vilivyo kwa udi na ambari na mabawa lazima haki itunzwe ili isipokonywe au isiponyoke kwani mwanaume inajulikana akiwa hivyo
- Mata- Kifo
Maizi- Cha manufaa/ dhamana
Fususi-Mchungaji
USHAIRI WA 7
6. i) Una moyo gani N’nakuuliza Wangu mhisani
Na kiasi gani Unavyojiweza Ijapo tufani
Ukiwa laini Utajipoteza Usijibani
Kusimama Pweke Kwataka Makini
ii) Zitavuma pepo Zitapupuliza Uanguke chini
Ela uwe papo Unajikweleza Na kujiamini
Utikiishapo Umejiuiza Pigo la moyoni
Kusimama Pweke Kwataka Makini
iii) Utie migati Ya kutuoteza Hapo aridhini
Kwa nia na dhati Usiogeuza Au kuihini
Zidate baruti Uwe wapuuza Welele usoni
Kusimama Pweke Kwataka Makini
iv) Sishike vishindo Na mauzauza Ya kukuzaini
Kita kama nyundo Ukinuiliza Unayoamini
Na uje mkondo Utadikimiza Kujipa mizani
Kusimama Pweke Kwataka Makini
v) Wengine wasiwe Unaoweleza Yaliyo maani
Wewe ndiwe Unaoweleza Yaliyo maani
Ela kichukuwe Pia kujikaza Katika midani
Kusimama Pweke Kwataka Makini
a) Lipe kichwa shairi hili (al 2)
b) Kwa nini kusimama pweke “kwataka makini ’’ (al 2)
c) Ni hatua gani zinazopendekezwa mtu anayenuia kusimama pweke? (al 5)
d) Andika arudhi za shairi hili (al 5)
e) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi hili (al 6)
- Muhisani
- Migati
- Vishindo
- Kweleza
- Mizani
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 7
6. a) – Upweke wataka umakini
– Upweke ni uvundo (al 2)
b) – Kwasababu matatizo au shida zinapomsonga mtu, asipokuwa na utulivu wa fikira basi – “Yeye huvunjika moyo” kwa vile hapana mtu wa kushirikiana naye (al 2)
c) – Mtu anastahili kuwa mwenye moyo mgumu/ wa ujasiri
– Awe tayari kusimama kwa udhabiti pindi shida zinapomkabili
– Ajiamini kwa lolote atendalo kwa imara
– Awe si mtu wa kutenda mambo ovyo ovyo ambayo yanaweza kumshawishi akaingia mtegoni
– Awe mstahimilivu na mwenye msimamo dhabiti
– Awe tayari kudinda na siri za ndani
d) i) Lina beti tano
ii) Kila ubeti una mishororo minne, minne
iii) Ukawafi- Lina vipande vitatu- ukwapi, utao na mwandamizi
iv) Kila kipande kina mizani 6, jumla 18 kila mshororo
v) Kibwagizo chenye kimefupishwa mizani 12
vi) Vina vya ukwapi vinabadilika badilika. Vina vya utao na mwandamizi
vinatiririka
e) Mhisani – Mtu mwema
Migati – Vizuizi
Mkindo – Mw
Unajikweleza –
USHAIRI WA 8
Soma shairi lifuatalo na kisha ujibu maswali yafuatayo.
UKUBWA JAA
Dunia yetu dunia, watu wanakufitini, Dunia huna udhia, watu wanakulaani, Dunia huna hatia, wabebeshwa kila zani, Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia umenyamaza, umetua kwa makini, Dunia vitu mejaza, watu wanataka nini? Dunia wanakucheza,binadamu maluuni, Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia mtu akose, hukutia mdomoni, Dunia hebu waase, hao watu mafatani, Dunia chuki mpuse, muipate afueni, Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia una lawama, za uongo si yakini, Dunia wanokusema, ni manjunju si razini, Dunia huna hasama, waja ndio kisirani, Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia kuharibika, hayo amezusha nani? Dunia watu humaka, hao wanokuhini, Dunia umejazika, kila tunu ya thamani, Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia unatukisha, bwerere bila undani, Dunia unatukosha, maji tele baharini, Dunia unaotehsa, mimea tosha shambani, Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia hujageuka, tangu umbwe na manani Dunia watu ndo, nyoka, mahaini na wahuni Dunia una baraka, mwenye pupa hazioni Dunia huna ubaya, wabaya ni insani.
Maswali:
(a) Shairi hili ni la bahari gani? Toa sababu yako. (alama 3)
(b) (i) Kichwa cha shairi hili kinaoanaje na maudhui ya shairi?. (alama 2)
(ii) Andika methali moja inayoeleza maudhui ya shairi hili. (alama 3)
(c)Eleza sifa tatu za wanadamu kama anavyoeleza mshairi. (alama 3)
(d)Kwa kutoa mifano kutokana na shairi hili, eleza mbinu tatu za lugha alizotumia
mshairi. (alama 6)
(e) Eleza maana ya vifungu vifuatavyo vya maneno kama vilivyotumika katika shairi.
(i) bwerere bila undani
(ii) hao watu mafatani
(iii) afueni
(iv) insani (alama 4)
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 8
1.
(a) Ni bahari ya kikwamba neno dunia limerudiwa mwanzoni mwa kila mshororo. Bahari nyingine ni ukara, kwa kuzingatia mwanzo, mloto, na mleo, vina vya ukwapi vinabadilika bali cha utao hakibadiliki. Pia, kuna manthawi, mistari ina ukwapi na utao (vipande viwili).
(b) (i) Kutokana na ukubwa wake, dunia inatupiwa lawama kwa maovu, udhia na hatia za kila
aina. Dunia inalinganishwa na jalala la kutupia taka.
(ii) Mbaazi ukikosa kuzaa husingizia jua.
(c) Binadamu hawapendi kulaumiwa.
Wana kisirani
Ni wahuni, wahaini
Ni waongo.
(d) Mbinu za lugha:-
Takiri – neno dunia limerudiwarudiwa na pia kibwagizo.
Dunia umeonewa, umetenda kosa gani?’
Tashhisi – Dunia imehuishwa kama mfano:- “Dunia hebu waase inaombwa itoe
mawaidha kwa walimwengu. Isitiara – ‘Dunia watu ndo nyoka’.
Watu wanalinganishwa na nyoka
(e) Maana ya vifungu:
Bwerere – bila undani – bure pasipo chuki, kinyongo.
Hao watu mafatani – hao watu wafitini
Afueni – nafuu, afadhali
Insani – watu, binadamu.
USHAIRI WA 9
1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Jama, Jama, Jamani
Mbona twabebeshwa mateso hivi
Mizigo mikubwa ya dhiki kama
Kwamba hatuna haki ya kusema
Kukataa ndoa za lazima
Kukataa kuozwa wazee
Kukataa kukatishwa masomo
Kukataa tohara ya lazima
Jama, Jama Jamani
Iweje tuteswe mateso haya
Na watu wasio kuwa hata na haya kama
Kwamba hatuna haki ya kulalamika
Kulalamikia kutumikishwa kama mayaya
Kulalamikia kudhalilishwa kiunyama
Kulalamikia kutolindwa na sheria
Jama, Jama, Jamani
Sasa hii ni awamu nyingine
Na macho tumeyafungua kabisa
Tumekataa kudhalilishwa kabisa
Tumekataa kuteswa kama watumwa
Tumekataa tohara ya lazima
Tumekataa kuozwa……. Tumekataa! Tumekataa
Hii awamu ya ’Haki ya mtoto wa kike’
Maswali
a) Taja mambo matatu muhimu yaliyozungumzwa na mshairi kisha ueleze kila
moja. (Alama 6)
b) Eleza muundo wa shairi hili (Alama 4)
c) Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi kisha ueleze kila moja(Alama 4)
d) Kwa nini mshairi huyu anasema hii ni ’awamu’ nyingine? (Alama 3)
e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa na mshairi (alama 3)
- awamu
- kudhalilishwa
- Dhiki
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 9
- a) SHAIRI
Mambo matatu muhimu yaliyozungumziwa na mshairi na maelezo ya kila moja.
Kutaja alama 1
Kueleza alama 1
Jumla ( alama 6)
i) Mateso
-Mizigo mikubwa ya dhiki
-Hakuna haki ya kunena
ii) Ndoa ya lazima
-Kuozwa kwa wazee
-Kukatishiwa masomo
iii) Tohara
-Tohara ya lazima
-Hawaruhusiwi kusema chochote
iv) Sheria
-Haiwalindi
-Kudhalilishwa kinyama
v) Awamu tofauti
-Wamekataa kudharauliwa
-Wamekataa kuteswa
-Wamekataa tohara za lazima.
- Muundo wa shairi
i)Ni wimbo ambao haufuati muundo wowote wa ushairi
ii)Ni shairi huru
iii)Halina mpangilio wowote wa kiarudhi
iv)Halina mgao wa mishororo
v)Halina vina wala mizani
vi)Halina kibwagizo
vii) Lina beti 3
viii)Mishororo si sawa katoka kila ubeti
c. Mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi. Maelezo ya kila moja
i) Nyimbo-Amezitumia Kwa njia mwafaka ili anase hisia za wasomaji.
ii) Takriri-Amejaribu pia kusisitiza ili kuwekea uzito yale anayozungumzia.
-Anataka msomaji apate mvuto mzuri kwa lile analolizungumzia. Mfano tumekataa kudhalilishwa, tumekataa kuteswa, tumekataa tohara.
iii) Mdokezo. Mfano Tumekataa kuozwa …
iv) Tashbihi . mfano ubeti wa pili- Kutumikishwa kama yaya
d. Sababu za mshairi kusema; ‘hii ni awamu nyingine’
i)Ulikuwa ukurasa mpya wa maisha.
ii)Kuna mabadiliko ya kuondoa ukandamizaji.
iii)Wanawake wamekataa kuozwa kwa lazima.
iv)Wamekataa kudhalilishwa kabisa
e. Maana ya maneno
i)) awamu-Kipindi
ii) kudhalilishwa-kukandamizwa/ kudunishwa / kufedheheshwa
- dhiki-shida
USHAIRI WA 10
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo
- Mkata ni mkatika, harithi hatoridhiwa
Sina ninalolishika, wala ninalochukuwa
Mlimwengu kanipoka, hata tone la muruwa!
Mrithi nini wanangu?
- Sina ngo’mbe sina mbuzi, sina konde sina buwa
Sina hata makaazi, mupasayo kuyajuwa
Sina mazuri makuzi, jinsi nilivyoachwa
Mrithi nini wanangu?
- Sina kazi sina bazi, ila wingi wa shakawa
Sina chembe ya majazi, mno nikukamuliwa
Nakwa’cheni upagazi, ngumu kwenu ku’tuwa
Mrithi nini wanangu?
- Sina sikuachi jina, mkata hatasifiwa
Hata nifanye la mana, mno mi kulaumiwa
Poleni wangu sana, sana kwenu cha kutowa
Mrithi nini wanangu?
- Sina leo sina jana, sina kesho kutwaliwa
Sina zizi sina shina, wala tawi kuchipuwa
Sina wanangu mi sina , sana la kuacha kuraduwa
Mrithi nini wanangu?
- Sina utu sina haki, mila yangu meuliwa
Nyuma yangu ili dhiki, na mbele imekaliwa
N’nawana na miliki, hadi nitakapofukiwa
Mrithi nini wanangu?
- Sina ila kesho kwenu, wenyewe kuiongowa
Muwane kwa nyinyi mbinu, mwende pasi kupumuwa
Leo siyo kesho yenu, kama mutajikamuwa
Mrithi nini wananngu?
- Taja mambo yoyote mawili ambayo mtunzi angewarithisha wanawe. (alama 2)
- Eleza sababu ya mtunzi kutoweza kuwarithisha wanawe. (alama 3)
- Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 4)
- Dondoa mifano miwili miwili ya : (alama 2)
- Inkisari
- Tabdila
- Chambua shairi hili kwa upande wa :
- Dhamira (alama 2)
- Muundo (alama 4)
- Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumiwa katika shairi. (alama 3)
- Mlimwengu kanipoka
- Sina konde sina buwa.
- Wingi wa shakawa.
- Mlimwengu kanipoka
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 10
- – Makazi mabovu
– Upagazi
– Kutothaminiwa
– Dhiki
– Kufanya kesho ya wengine nzuri
- – Ni maskini hohehahe / hana kitu
– Aliporwa kila kitu.
– Hana mifugo.
– Hana kazi yoyote.
– Hana sifa / umaarufu.
– Ana makazi mabovu.
- – Sina jina nitakawacha kwani maskini hasifiwi
– Hata nikifanya jambo la maana ninalaumiwa tu.
– Poleni sana wanangu kwa kuwa sina la kuwatolea.
– Mtarithi nini wanangu?
- (i) Inkisari
- Mana – Maana
- Meuliwa – Imeuliwa
- Nitapofukiwa – Nitakapofukiwa.
(ii) Tabdila
Muruwa – Murua
Kutowa -Kutoa
Kuchipuwa -Kuchipua
Kuiongowa – Kuiongoa
Kupumuwa – Kupumua
- (i) Dhamira
- Kuwahimiza watu kufanya bidii wakiwa vijana.
- Kulalamika kwamba maskini hana haki / huonewa / hapewi nafasi.
(ii) Muundo
- Shairi ni aina ya tarbia / unne.Lina mishororo minne katika kila ubeti.
- Mishororo ya kwanza mitatu imegawika katika sehemu mbili (ukwapi na utao).
- Kila kipande kina mizani nane na kila mshororo una mizani kumi na sita.
- Vina vya kati vinatofautiana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine, lakini vina vya mwisho ni sawa katika shairi zima katika mishororo ya kwanza mitatu.
- Shairi hili lina kibwagizo ambacho kimefupishwa.
Mrithi nini wanangu?
- Shairi hili lina beti saba.
- (a) Mlimwengu kunipoka – Mlimwengu kanipokonya.
(b) Sina konde sina buwa – Sina shamba sina chochote.
(c) Wingi wa shakawa – mashaka mengi.