KCSE Predictions Ushairi Questions And Answers- Shairi 6-10
KCSE Predictions Ushairi Questions And Answers- Shairi 1-5
USHAIRI WA 16
Vita vya ndimi
Huyo! Amshike huyo!
Hakuna bunduki wala kifaru
Bomu na risasi hata hawazijui!
Lakini mno wanashambuliana.
Kwa ndimi zilizonolewa kwa makali
Vipande vya matusi silaha zao.
Yu imara mmoja wao.
Akirusha kombora la neno zito!
Limtingishe adui wake
Na kumgusa hisia kwa pigo kuu.
Pigo linalopenya moyoni kama kichomi
Kuchipuza joto la hasira na kisasi
Katika mapigano yaso na kikomo.
Filimbi ya suluhu inapulizwa kuwaamua!
Ni nani anayekubali suluhu?
Roho zinakataa katakata
Huku ukaidi ukinyemelea na kutawala kote
Mapandikizi ya watu yakipigana
Vitu shadidi visivyo ukomo
Vita vya ndimi!
Magharibi sasa
Jua linapungia mkono machweo
Nalo giza likinyemelea kwa kiburi na kasi
Sisikii tena sauti za misonyo
Mate ya watesi yamekauka
Makanwa yao yamelemewa na uchovu
Sasa wameshikana mikono
Nyuso zao zikitabasamu
Ishara ya suluhu!
- Hili ni shairi la aina gani? (alama 1)
- Eleza sifa za utunzi alizotumia mshairi. (alama 4)
- Taja kwa kutolea mifano tamathali za usemi zozote tatu zilizotumiwa katika shairi hili.(alama 3)
- Fafanua mishororo hii:
- Akirusha kombora la neno zito!
- Makanwa yao yamelemewa na uchovu (alama 4)
- Zungumzia mgogoro katika shairi na namna unavyomalizika. (alama 6)
- Toa maana ya msamiati huu
- Kichomi
- Misonyo (alama2)
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI 16
1. (a) (i) Shairi huru.
- Shairi la kimapindusi.
- Sakarani.
(b) Sifa za utunzi. (muundo umbo)
- Shairi lina beti nne.
- Idadi ya mishororo inatofautiana katika beti za shairi.
- Halina mpangilio maalum wa mizani.
- Halina vina (masivina)
- Halina kibwagizo.
- Beti zake hazijagawanywa katika vipande.
Zozote 4×1=4
(c) Tamathari za msemi.
- Nidaa/siyali/mshangao.
Km. Huyo! Amurike huyo!
- Balagha.
Km. Ni nani anayekubali suluhu?
- Tashbihi.
Km. Pigo linalopenya moyoni kama kichwani.
- Takriri.
Km. Roho zinakataa kata kata.
- Tashhisi
Km. Jua linapungia mkono machweo.
- Istiari
Km. Kuchipuza joto la hasira na kisasi.
Zozote 3×1=3
(d)
- Akimsha kumbora la neno zito!
Akitoa matusi ya kuudhi/kukasirisha.
- Makanwa yao yamelemewa na uchovu.
Midomo yao haitoi matusi tena (imetulia)
(2×2=4)
(e)Mgogoro:
- Kuna vitu vya maadui wawili.
- Wanapigana kwa midomo yao – wanatusiana
- Matusi yenyewe ni makali mno.
- Matusi yanaleta hasira/hamaki kwa anayetusiwa.
- Ingawa kuna juhudi za kuwapatanisha wanakataa kabisa.
- Wanazidi kuwa wakaidi na kuendeleza vita vyao vya matusi.
Zozote 4×1=4
Kumalizika
- Jioni inapofika, wamechoka ndipo wanatulia.
- Wanaridhiana (wanashikana mikono) huku wakitabasamu na kusameheana.
Zozote 2×1=2
(f)
- Kichomi – lenye kuumiza
- Misonyo – mifyonyo, kufyonya kwa hamaki au ishara ya chuki.
USHAIRI WA 17
Soma mashairi ya A na B kisha ujibu maswali.
A
Mtu ni afya yake, ndio uzima wa mtu
Mtu ni kuwa na chake, hakuwi ela kwa kitu
Mtu ni bahati yake, kupendekeza kwa watu
Mtu si fakhari kwako, kuitwa nyama ya mwitu
Mtu ni ulimi wake, kunena vyema na watu
Mtu ni kijungu chake, kuweka mawe matatu
Mtu ni mwenda kwa lake., mtoshawa na kula kitu
Mtu si uzuri kwake, kuitwa nyama wa mwitu
Mtu ni mwenye nadhari, apimaye kula kitu
Mtu ni moyo hariri, mwenye imani na watu
Mtu ni alo na ari, shika sana mwana kwetu
Mtu si yake fakhari, kuitwa nyama wa mwitu
Mtu ni mkono wazi, mtasadaku na watu
Mtu ni mwenye maozi, kuoneya kula kitu
Mtu ni alo tulizo, asopenda utukutu
Mtu si jambo pendezi, kuitwa nyama wa mwitu
Mtu ni mwenye ahadi, ndio u’ngwana na utu
Mtu ni alo baridi, mbembeleza wa watu
Mtu ni moyo asadi, asoonewa na mtu
Mtu si yake ifadi, kuitwa nyama wa mwitu
Mtu niliyoyanena, pima sana ewe mtu
Mtu sikuja tukan, kukirihi nyoyo watu
Mtu nakupa maana, wende nyendo za kiutu
Mtu si uzuri sana, kuitwa nyama wa mwitu
Mtu ni mtenda njema, atwiiye Mola wetu
Mtu ni mbele na nyuma, pima sana mwana kwetu
Mtu natiye khatima, fafanua kula kitu
Mtu si yake hisima, kuitwa nyama wa mwitu.
B
MTU HACHAGUI KAZI
Naamba kazi ni kazi, vyovyote vile iwavyo
Madamu si ubazazi, kwa mwanaadamu ndivyo
Kushona na upagazi, pia vile vyenginevyo
Kazi ni kitu azizi, wala vyenginevyo sivyo
Mtu hachagui kazi.
Mtu hadharau kazi, ile ahisiyo duni
Ayuzuie machozi, walilia jambo gani
Ukulima na ukwezi, na uvuvi baharini
Hizi nazo njema kazi, yafaa uzibaini
Mtu hachagui kazi
Si laiki kubughudhi, hakuna iliyo duni
Hayo makubwa maradhi, na tena uhayawani
Kazi zote zina hadhi, hivyo tusibagueni
Inafaa tuziridhi, tuzitende kwa yakini
Mtu hachagui kazi.
Ni wajibu kuipenda, na kuikiri moyoni
Na kwa dhati kuitenda, kwa juhudi na makini
Matatizo huyashinda, na uvivu kuuhuni
Hapo mtu atashinda, na magumu kumhuni
Mtu hachagui kazi
MASWALI
- Lipe shairi la A kichwa mwafaka. (alama 1)
- Kwa mifano mwafaka fafanua bahari katika shairi la A na B. (alama 4)
- Toa sababu za mwandishi kuchagua “Mtu hachagua kazi” kama kichwa cha shairi la B.
(alama 1)
- Mtunzi alikuwa na ujumbe gani katika mashairi haya? (alama 4)
- Andika ubeti wa pili wa shairi A katika lugha nathari. (alama 4)
- Eleza muundo wa shairi la B. (alama 4)
- Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika mashairi haya. (alama 2)
(i) Nadhari
(ii) Ubazazi
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA USHAIRI WA 17
- Mtu si mnyama wa mwitu (alama 1)
- Shairi A
- Kikwamba – neon la kwanza katika kila mshororo ni sawa – mtu.
- Ukara – kina cha mwisho hakibadiliki huku cha kati kikibadilika
2 x 1 = 2.
Shairi B
- Msuko – mshororo wa mwisho wa kila ubeti umefupishwa.
- Ukaraguni – vina vya kati na vya mwisho vinabadilikabadilika.
2 x 1 =2.
- Ni kibwagizo na kinabeba uzito wa ujumbe unaozungumziwa.Alama 1.
– Mtu anatakikana kutenda mazuri kila wakati.
– Kazi zote ni nzuri kwa hivyo tusiwe watu wa kubagua kazi
2 x 1 = 2.
– Mtu hujulikana kwa yale anayosema yeye na watu wengine.
– Ni mtu mwenyewe kujijenga.
– Mtu ni yule anayetumia chake na kutosheka nacho.
– Si jambo zuri mtu kuitwa mnyama wa mwituni.
4 x 1 = 4.
- Shairi B
– Beti nne (4)
– Mishororo mitano kila ubeti.
– Mizani kumi na sita kila mshororo.
– Kibwagizo kimefupishwa.
– Kuna vipande viwili, ukkkwapi na utao.
– Vina vinabadilika badilika.
4 x 1 = 4.
- Nadhari – busara
- Ubazazi – ulaghai
USHAIRI WA 18
Soma shairi lifuatalo kisha uiibu maswali
Duniani husifiki;
Wala hupati thamani,
Yalisemwa hukumbuki?
Na wazee wa zamani,
“Mkono haurambiki,
Bila kitu kiganjani”
Wangapi watu azizi,
Fulani bin Fulani,
Waliokichinja mbuzi,
Kukirimu mitaani,
Sasa kama wapuuzi,
Kwa hali kuwa ta’bani
Walifanya makubeli.
Wakaapa hadharani,
La uongo huwa kweli,
” Kubishika kitaani,
Na tangu kukosa mali,
Wakawa kama nyani!
Walifanya mahashumu.
Kuwaliko masultani,
Ushekhe na Ualimu,
Kufasiri vitabuni,
Na leo wana wazimu,
Kama si wanachuoni.
Maswali
(a) Kwa maneno yako mwenyewe eleza ujumbe wa shairi hili. (Alama 3)
(b) Eleza jinsi mshairi anavyosisitiza huo ujumbe katika shairi lote. (Alama 4)
(c) Eleza kwa tafsili umbo la shairi hili. (Alama 5)
(d) Andika ubeti wa kwanza katika lugha nathari. (Alama 3)
(e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyo tumika katika shairi;
(i) Kiganjani.
(ii) Kukirimu.
(iii) Makubeli.
(iv) Mahashumu.
(v) Wanachuoni (Alama 5)
USHAIR1:
Soma shairi lifuatalo kisfea ujibu saaswali vanavofuata:
1.
Niliusiwa zamani, babu aliniusia, N
ili bado utotoni, hapo aliponambia,
Babu yaweke kitwani, yasije yakapotea,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
2. Wewe bado ni mgeni, katika hii dunia,
Mimi ndiye wa zamani, mengi nimejionea,
Sasa niko uzeeni, uzee umewadia,
penye nia ipo njia, usikate tumaini.
3. Mtima ndio sukani, waongoza’kila ndia,
Weka mkazo moyoni, kila unalofwatia,
Moyoni mwako amini, kuwa utalifikia,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
4. Kama uko safarini , waongoza kila ndia,
Bahari kuu kinani, mawimbi yakuchachia,
Usikate tumaini. hapo ndipo penye ndia,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
5. Hapo hapo mawimbini, wewe hapo pigania,
Hapo ndipo milangoni, mawimbi yakuzuia,
Mtima utie kani, bandarini utangia,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
6. Na iwapo ni shuleni, masomo yakutatia,
Usiasi masomoni, kusoma ukakimbia,
Kidogodogo bongoni, elimu itakungia,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
7. Kama wenda uchumini, biashara waania.
Usihofu asilani, hasara ikitukia,
Leo ukipata duni, na kesbo litazidia,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
- Andika methaii ambayo ingetumiwa kujumuisha ujumbe katika ubeti wa pili. (Alama 1)
- Kutokana na shairi hili, ni katika nyanja zipi za maisha tunapopaswa kujikakamua? Tujikakamue vipi? (alama 6)
- Taja arudhi ambazo zimetumiwa kuusarifu ubeti wa kwanza. (Alama 4)
- Huku ukitoa mfano mmoja bainisha uhuru wa kishairi ambao umetumiwa katika ubeti wa 3.
(alama 1)
- Andika ubeti pili kwa lugha ya nathari. (Alama 4)
- Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi.
- Aliniusia.
- Mtima.
- Sukani
- Waania. (Alama 4)
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA USHAIRI WA 18
- (a) Mshairi anasemaa kuwa mtu ambaye hana mali hadhaminiwi kwa kuwa mkono mtupu haulambwi. ( alama 3)
(b)
- kwa kueleza vile Sultan, Shehe, walimu walivyopungua thamani.
- Kwa kutumia methali; mkono mtupu haulambwi
- Kwa kutumia methali, tashbihi za kinyume mfano
Azizi kuwa kama wapuuzi
Makubeli kuwa kama nyani. (alama3)
(c) Umbo la shairi
- Ni shairi huru
- Tasdisa / usita/ utenzi/ shairiguni (ubeti 3- Baheri ina mzani saba.) Pia zuhali (mtiririko) Kwa vina vyenye irabu yenye keketo i isipokuwa ubeti wa mwisho wenye irabu u.
- Kila mshororo una kina kimoja tu cha nje (kipande kimoja)
- Vina havina urari.
Maelezo yoyote kuhusu vina
Ubeti:
- ki, ni,ki,ni,ki,ni.
- zi,ni,zi, ni,zi,ni
- li,ni,li,ni,li,ni.
- mu,ni,mu,ni,mu,ni.
- Lina kituo kinacho badilikabadilika
- Mizani: nane kila mshororo
- Idadi ya beti –nne. (zozote 5×1=5)
(d) Mshairi anasema kuwa duniani hatambuliwi (hathaminiwi). Anatukumbusha kuwa wahenga walisema ‘mkono mtupu haulambwi.’ Kwamba duniani ukiwa huna kitu basi huthaminiwi. (Alama 4)
(e) (i) Kiganjani – mkononi /kitangani.
(ii) Kukirimu – kufanya wema, kufadhili fanyia hisani.
(iii) Makubeli- watukufu/ wanadhama /wenye vyeo/ wakubwa.
(iv) Mahashumu – waheshimiwa / makubeli / watukufu.
(v) Wanachuoni – waeledi /wajuzi / wataalamu /wasomi.
7. (a) Kuishi kwingi ni kuona mengi (alama 1)
(b) Safarini – matatizo yakizidi tusipoteze tumaini kwani huwa tumekaribia kufanikiwa.
- Masomoni – masomo yakiwa magumu tusiache kusoma, tuuhimize ubongo mpaka uitikie.
- Katika biashara – hasara ikiingia tusione kama tumefika mwisho. Kufaidika na kuhasarika ni kawaida katika biashara (alama 6)
(c) ubeti una mishororo minne (tarbia)
- Kila mshororo una vipande viwili, ukwapi na utao.
- Mpangilio wa vina .
_______ni __________ a
_______ni___________a
_______ni___________a
________a__________ni
Mizani
________8________8
________8________8
________8________8
________8________8
Kibwagizo ni: penye nia ipo njia, usikate tumaini. (alama 1)
- Mazida- kurefusha maneno k.m “Usikate” tumaini ya “ sikate”
Lahaja kitwani badala ya kichwani
ndia badala ya njia, n.k.
Inkisari – unalofwatia badala ya “ unalolifuatia”
Kubadili sauti/ kuboronga sarufi – penye nia ipo njia – moyoni mwako amini (Tabdila)
Kubainisha ½
Mfano ½ (alama 1)
(e)
- Mshairi ana umri mdogo na hajazoea vituko vya dunia.
- Babu amekula chumui nyingi na ameona mengi.
- Sasa ni mzee kwani ana umri mkubwa.
- Palipo na matumaini hapakosi mafanikio kwa hivyo asikate tamaa.
(alama 4)
- Aliniusia – alinishauri
- Mtima –moyo
- Sukani – kiongozi
- Waania – shindania (alama 4)
USHAIRI WA 19
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata
Kaka: Kusoma nilikosoma, kambiwa sipati kazi,
Yapata mwaka mzima, nategemea shangazi,
Wasiojuwa husema, ‘ sababu sina ujuzi,’
Huno uhaba wa kazi, mesababishwa ni wake.
Dada: Mbona watuingilia, kaka acha ubaguzi,
Likukeralo twambia, tulijuwe waziwazi,
Au unalochukia ni wake kufanya kazi?
Mambo ya siku hizi,watu ni bega kwa bega.
Kaka: Siwangilie kwa nini, nanyi mwatukopa kazi
Kwani tokea zamani, hazikuwa shida hizi,
Mtu kitoka shuleni, kibaruwa si tatizi,
Leo hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake
Dada: Hapo kaka hujasema, kuwa wake ndiyo chanzi,
Chanzo cha hii nakama, waume kukosa kazi,
Bure mwatupa lawama, wenyewe mna ajizi,
Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.
Kaka: Hayo unayotamka, yote niya upuuzi,
Mumetoroka kupika, kazi yenu toka enzi,
Bilashi mwahangaika, kushabihi vijakazi,
Sasa hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake.
Dada; Mbona wafanya ukali, ishakuwa ni chukizi?
Hata na yangu kauli, umekuwa husikizi,
Nisemaye ni halali,ukweli uliowazi,
Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.
Kaka: Yana uhalali gani, mbona basi huelezi?
Kipita maofisini, mumejaa kama inzi,
Mwataka tuwe mekoni, wala halitupendezi,
Na nje hakuna kazi, kisa nyinyi wanawake.
Dada: kakangu una matata, kuyaelewa siwezi,
Wasema unamopita, wambiwa hakuna kazi?
Na sisi wake twapata, haraka pasi ajizi,
Sababu siku hizi, watu ni bega kwa bega.
Kaka: Sisi kazi hatupati, wengi wetu ni mijizi,
Elanyi muna bahati, mabosi hawawaizi,
Hampotezi wakati, ni kidogo pingamizi,
Nasi hatupati kazi, kisa nyingi wanawake..
Dada: kakangu wanichekesha, hadi sina kizuizi,
Vipi lakukasirisha, sisi tukifanya kazi?
Hujui ndivyo maisha, yaendavyo siku hizi?
Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.
Kaka: Huna haja ya kucheka, nisemayo si upuzi,
Kazi inayojulika, yenu ni kukuna nazi,
Kisha mwenda zianika, mukaziuze takizi,
Leo hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake.
Dada: Yalikuwa ni ya kale, kuuza chicha za nazi,
Ela leo twenda mbele, na nyuma hatujibanzi,
Hakuna aliyelele, kushiriki usingizi,
Kwani mambo siku hizi, watu ni bega kwa bega.
Kaka: kulla kitu mwakitaka, kiwe chenu siku hizi,
Ishakuwa na miaka, pia mwataka ihozi,
Nasikia mwatamka, mwaka huno wa ledizi,
Mwisho mutataka myezi, iwe yenu wanawake.
Hai mana kubishana, nikashabihi mkizi,
Mengi niliyoyanena, yafanyie uchunguzi,
Iwapo tutafanana, yupi taleya vizazi?
Sisi hatupati kazi, hadi murudi mekoni.
Dada: Baba mbele mama nyuma, yamekuwa simulizi,
Muradi sote twasoma, soteni tuwe walezi,
Wake haturudi nyuma, tunataka mapinduzi,
Maisha ya siku hizi, watu ni bega kwa bega.
MASWALI
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (Alama 2)
b)Dada anatoa sababu gani ya wanawake kuajiriwa maofisini? (Alama2)
c) Kaka anataja sababu zipi za wanaume kukosa kuajiriwa kazi? (Alama2)
d) Eleza umbo la shairi hili (Alama3)
e)Dondoa na ueleze mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika shairi (Alama4)
f) Kwa mujibu wa shairi hili, kazi za wanawake ni zipi? (Alama2)
g) Eleza ubeti wa mwisho kwa maneno yako mwenyewe (Alama2)
h) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi. (Alama3)
(i) Kulla
(ii) Nakama
(iii) Ajizi
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA USHAIRI 19
a) i) Uhaba wa kazi
ii) Ukosefu wa kazi
iii) Wanaume kubaguliwa kazini ( 1x 2 =2)
b) – Miasha ya siku hizi yanahitaji waume na wake, ni sawa kufanya kazi bega kwa
bega. ( 1 x 2=2)
c) i) Wanawake wameingilia kazi za wanaume
ii) Wanawake kupata kazi ni rahisi kuliko waume kwa sababu wakuu wanawaajiri
kwa maslahi yao wenyewe ( 2 x 1= 2)
d) i) Ngonjera – majibizano
ii) Tarbia – mishororo minne kwa kila ubeti
iii) Ukara – vina vya nje vyatiririka ilhali vya utao vyabadilikabadilika iv) Takriri – ‘Kisa nyinyi, wanawake’ na ‘watu ni bega kwa bega.
( 3 x 1 = 3)
- (Kutaja – alama 1 na kueleza alama 1)
- Kuvuruga / kubananga / kufinyanga sarufi
k.m. – likukerelo – linalokukera
– Soteni – Sote
- Tabdila (kubadilisha heruf kimaksudi)
k.m. – Inzi – nzi
– Kulla – kila
– tulijuwe- tulijue
- Inkisari
– Kipita – nikipita
– Kitoka – akitoka
– elanyi – ela nyinyi.
- Kutumia maneno ya lugha nyingine au lahaja
k.v – ledizi
– aliyelele
– kula ( 2 x 2= 4)
f) i) Kupika
ii) kukuna nazi (kazi za mekoni)
iii) kuzaa na kulea wana. ( 2 x 1 = 2)
- Mambo ya kuwekwa (kutangulizwa) baba au wanaume mbele na wanawake wawe
nyuma yameisha. Maadamu (kwa vile ) sote sisi waume kwa wake tunapata elimu
pamoja – basi vilevile sote tuwe walezi wa watoto. Tusibaguliwe. Moja ikawa kazi
ya mtu mmoja tu.
Wanawake tutapigana mpaka tupatiwe haki yetu ya usawa. Lazima kupatikane mabadiliko. Maisha ya siku hizi watu wote lazima wawe pamoja, wafanye kazi sawa.
( alama 2)
- i) Kulla – kila 1
ii) Nakama- maangamizo, gharika 1
iii) Ajiri – ugoigoi,ulegevu, uzembe 1
USHAIRI WA 20
Soma shairi hili kasha ujibu maswali.
1. Pasi kuhofu lawama, imenibidi kunena,
Nina mengi ya kusema, ambayo ni ya maana
Kwetu sote ni lazima, viumbe kuambizana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
2. Sahau I akilini, yataka kukumbushana,
Madamu tu duniani, la kosa huelezana,
Ili tuwe hadharini, tujilinde na fitina,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema
3. Uchochezi ukitiwa, uwongo unapofana,
Lolote laweza kuwa, hata watu kupigana,
Fitina yaweza ua, binadamu wengi sana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
4. Fatani anapojua, jamii yasikizana,
Aweza leta adawa, ya fitina kugombana,
Hata akawa baguwa, ndugu wakafarikana,
Yashinda kifo fitina, fatani si ntu mwema.
5. Nahakikisha wenzangu, fitina ina laana,
Fitina kwa Bwana Mungu, katu hataki iona,
Yasaliti walimwengu, mume mke kuachana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
6. Fitina si kitu safi, nazidi toa bayana,
Fitina ina makofi, muda ukijulikana,
Fitina ni ukorofi, mfano wake hapana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
7. Fitina yashinda tusi, uovu wa kutukana,
Fitina ina maasi, madhambi ya kujazana,
Fitina ina utesi, tena usowezekana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema
8. Fitina si masihara, yashinda hata khiana,
Fitina ina madhara, nchi zaweza gongana,
Fitina aina izara, na aibu nyingi sana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
9. Fitina haina shaka, ni mbovu nasema tena,
Fitina mali hakika, ya ghibu nawe waona,
Fitina ina mashaka, na dhiki kila namna,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
10. fitina kitu haramu, tamati zaidi sina,
Fitina na binadamu, wawe wakichukiana,
Fitina ni mbaya sumu, ya au sifa na jina,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu, mwema.
Maswali:
(a) Bainisha athari tanoza fitina kulingana na mshairi (alama 5)
(b) Ubeti wa sita umechukua mikondo na bahari tofauti tofauti. Zitaje na utoe mifano
(alama 4)
(c) Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nathari (kawaida) (alama 3)
(d) Mshairi ametumia mbinu zipi kufanya jumbe zake zieleweke kwa bayana zaidi.
(alama 4)
(e) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi.
(i) Adawa
(ii) Fatana
(iii) Wakafarikana
(iv) Tusi (alama 4)
Soma shairi hili kisha ujibi maswali yanayofuata.
1. Tusitake kusimama, bila kwanza kusimama,
Au dede kuwa hima, kabla hatujakaa,
Tutakapo kuchutama, kuinama inafaa,
Tujihimu kujinyima, makubwa kutoyavaa.
2. Tusitake kuenenda, guu lisipokomaa,
Tujizonge na mikanda, inapochagiza njaa,
Na mazuri tukipenda, ni lazima kuyandaa,
Tujiase kujipinda, kujepusha na balaa.
3. Tusitake uvulana, au sifa kuzagaa,
Tushikaye nyonga sana, tunuiyapo kupaa,
Kama uweza hapana, tutoelee dagaa,
Tujiase hicho kina, maji yajapokujaa.
4. Tusitake vya wenzetu, walochuma kwa hadaa,
Wanaofyatua vitu, na kasha vikasambaa,
Uwezo hatuna katu, umaskini fazaa,
Tujihimu kula vyetu, siendekeze tamaa.
5. Mtaka kuiga watu, kufata kubwa rubaa,
Vyao vijaile kwetu, vifaa vingi vifaa,
Tunamezwa na machatu, tusibakishwe dhiraa,
Tujihimu kilo chetu, hata kama twapagaa.
(a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)
(b) Eleza madhumuni ya shairi hili (alama 2)
(c) shairi hili ni bahari gani? Toa sababu. (alama 4)
(d) Bainisha umbo katika ubeti wa kwanza na wa mwisho ukizingatia vina na mizani.
(alama 4)
(e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari. (alama 4)
(f) Taja mbinu moja ya kisanii inayoibuka katika ubeti wa nne. Kwa nini
imetumiwa? (alama 2)
(g) Eleza msamiati ufuatao kama unavyotokea katika shairi. (alama 3)
(i) Kuiga
(ii) Dede
(iii) Tujizonge.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA USHAIRI WA 20
6 a) (i) Vifo
(ii) Vita
- Ugomvi / kuvuruga amani
- Talaka
- Ukorofi
- Chuki zozote 5×1=5
b) (i) Tarbia – Mishororo minne
(ii) Kikwamba- neno / kianzio kimerudiwarudiwa 2×2=4
- Mfitini agunduapo jamii yaelewana huleta utengano kwa kuingiza fitina.
Hata anaweza kuwatenganisha ndugu.
Mfitini ni mbaya kushinda kifo / mauti 3×1=3
d) (i) Jazanda – Fitina mbaya sumu
(ii) Takriri- Kibwagizo kurudiwarudiwa Neno fitina 2×2=4
e) i) adawa – uadui
ii) fatani – anayefitini
iii) wakafarikana – wakatengana, wakawa kando kando
iv) tusi – tukano. 4 x 1 = 4
7 a) Kujinyima.
Tusitake makuu. (Alama 1)
b) Kuhimiza msomaji asiwe na tamaa.
Kuonya dhidi ya kuwa na pupa. 1×2=2
c) Tarbia – mishororo minne kila ubeti
Ukara – Vina vya mwisho vinatiririka. 2×2=4
d) Umbo: ubeti ubeti 5
mizani 8,8 8,8
vina ma,a tu, a 4×1=4
e) Lugha sufufu.
Tusitamani kusimama kabla ya kutambaa au kabla ya kukaa.
Tunapotaka kuchutama ni lazima tuiname.
Tujifunze kujinyima yale ambayo hatuyawezi 4×1=4
f) Ritifaa – ‘siendekeze
Sababu- Kupata urari wa mizani 2×1=2
- Msamiati
(i) Kuiga – kufanya afanyavyo mtu mwingine
(ii) Dede – Imara, bila kushikilia kitu, bila usaidizi.
(iii) Tujizonge- Tujifunge, tujikaze. 3×1=3