1.SEHEMU A: USHAIRI (LAZIMA)– Kapsabet Boys
Eti
Mimi niondoke hapa
Niondoke hapa kwangu
Nimesaki, licha ya risasi
Vitisho na mauaji, siondoki
Mimi
Siondoki
Siondoki siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Kwa mateke hata na mikuki
Marungu na bunduki, siondoki
Hapa
Siondoki
Mimi ni Pahame!
Niondoke hapa kwangu!
Fujo na ghasia zikizuka
Na kani ya waporaji, siondoki
Haki
Siondoki
Kwangu siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Nawaje; waje wanaokuja
Mabepari wadhalimu, siondoki
Kamwe
Siondoki
Ng’oo hapa kwangu!
Katizame chini mti ule!
Walizikwa babu zangu, siondoki
Sendi
Nende wapi?
Si hapa kitovu changu
Niondoke hapa kwangu
Wangawa na vijikaratasi
Si kwamba hapa si kwangu, siondoki
Katu
Siondoki
Sihitaji karatasi
Niondoke hapa kwangu
Yangu mimi ni ardhi hii
Wala si makaratasi, siondoki
Maswali
a) Shairi hili ni la aina gani? Kwa nini (alama 2)
b) Taja masaibu anayopitia mzungumzaji (alama 4)
c) Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
d) Eleza muundo wa shairi hili (alama 3)
e) Tambua matumizi ya mbinu ya usambamba (alama 2)
f) Andika ubeti wa tano kwa lugha nathari (alama 4)
g) Tambua idhini moja ya mtunzi (alama 1)
h) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi (alama 3)
(i) Karatasi
(ii) Nimesaki
(iii)kitovu
2 SEHEMU B TAMTHILIA YA KIGOGO-Kapsabet Boys 2022
2.Uliona nini kwa huyo zebe wako ? Eti mapenzi!
a. Eleza muktadha wa dondoo. (al. 4)
b. Andika mbinu za lugha zinazojitokeza kwenye dondoo hili (al. 4)
c. Taja hulka za mnenaji unajitokeza katika dondoo. (al. 2)
d. Mwanamke ni kiumbe wa kukandamizwa. Thibitisha kauli hii ukirekjelea tamthilia. (al. 10)
3.wa kurejelea tamthlia ya ‘Kigogo ya Pauline Kea, onyesha jinsi ambavyo viongozi wengi katika nchi za kiafrika wamejawa na tamaa. (alama 20)
SEHEMU C. RIWAYA YA CHOZI LA HERI(ASSUMPTA MATEI)-Kapsabet Boys
4.“ Kwa kweli ni hali ngumu hii”
Weka dondoo katika muktadha wake. (alama4)
Ni hali gani yamsemewa inayorejelewa kwenye dondoo. (alama16)
5) Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za Kiafrika. Tetea kauli hii ukilejelea Chozi la Heri ( al. 20)
Alifa Chokocho na Dumu Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi nyingine
jibu swali la 6 au la 7
6.Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza. (alama20
a) Mapenzi ya kifaurongo
b) Masharti ya kisasa
c) Ndoto ya Mashaka
d) Mtihani wa maisha
Au
Shibe inatumaliza : Salma Omar Hamad
7.“Hiyo ni dharau ndugu yangu. Kwa nini kila siku tunakula sisi kwa niaba ya wengine ?”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b)Eleza sifa za msemaji. (alama 6)
c) Eleza jinsi viongozi wanavyokuwa wabadhirifu. (alama 10)
SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI -Kapsabet Boys
8a) Fafanua mchakato/fomula ya uwasilishaji wa vitendawili. (alama4)
b) Linganisha naulinganue vitendawili na methali. (alama10)
c) Toa sababu sita za kudidimia kwa fasihi simulizi. (alama6)