Swali la LAZIMA– Kassu Jet Kiswahili June 2022
Chamko la ugonjwa wa Korona lililemaza shughuli za michezo nchini. Wewe ni katibu wa jopokazi lililoteuliwa na Waziri wa Michezo kubuni mikakati ya kufufua michezo katika taasisi za elimu nchini. Andika kumbukumbu za mkutano huo.
- Vijana wamekuwa wakichelea kuhusika katika mchakato wa uchaguzi. Jadili vyanzo vya hali hii huku ukiwapendekezea vijana umuhimu wa kubadili msimamo huu.
- Tunga Kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo: Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
- Andika insha itakayomalizikia kwa:
…nilipotua nchini, nilishusha pumzi, nikamshukuru Jalia kwa kuponea chupuchupu katika uvamizi huo.