Get the Answers here Form 4 End Term 1 Exams 2023 Questions and Answers
SEHEMU A: (FASIHI SIMULIZI)
1. (a) Watu watatu walikuwa wakivuka mto. Mmoja alivuka pasi kukanyaga maji wala kuyaona.
Wa pili aliyaona maji akayavuka bila kuyakanyaga. Wa watatu aliyaona akayakanyaga
huku akiyavuka.
(i) Bainisha kipera cha makala hayo. (alama 1)
(ii) Eleza umuhimu wa kipera ulichotaja(i) hapo juu. (alama 4)
(b) Fafanua muundo wa mawaidha yanayotolewa katika miktadha rasmi. (alama 3)
(c) Fafanua sifa za mawaidha. (alama 12)
SEHEMU B: (TAMTHILIA) KIGOGO(PAULINA KEA)
2. …… kila mtu sagamoyo hafanyi kazi yakek – hata hao chatu! Kwa hivyo wataka niache raha
zangu, nijishike kichwa nilie?
(a) Eleza muktadha wa dondooo hili. (alama 4)
(b) Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 4)
(c) Kwa kutolea mifano mwafaka, angazia nafasi chanya alizopewa mwanamke katika tamthilia
ya Kigogo. (alama 12)
3. Mgala muue na haki umpe. Thibitisha ukweli wa methali hii ukimrejelea mhusika Husda.
(alama 20)
SEHEMU C: (CHOZI LA HERI) Assumpta K. Matei
4. “Nyamaza wewe! Nyinyi ndio mlioturudhisha nyuma miaka yote hii …….”
(i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4
(ii) Fafanua baadhi ya malalamishi ya msemaji wa kauli hii. (alama 6)
(b) Fafanua dhuluma dhidi ya watoto katika Riwaya ya Chozi la Heri. (alama 10)
5. Fafanua nafasi ya vijana katika jamii kwa mujibu wa Riwaya ya Chozi la Heri. (alama 20)
SEHEMU D: (HADITHI FUPI)
6. MAPENZI KIFAURONGO: Kenna Wasike
“Hadi sasa mimi ni kama rubani aliyeharibikiwa na ndege angani.”
Onyesha ukweli wa dondoo hili. (alama 20)
7. Ndoto ya Mshaka: Ali Abdulla Ali
Mwandishi wa hadithi hii anatupa taswira ya jamii iliyozongwa na masaibu
yanayotamausha. Tetea ukweli wa kauli hii. (alama 20)
SEHEMU E: (SHAIRI)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Weusi likosa nini?
1. Sie watu weusi, lipataje weusi?
2. Kila kitu kibaya, hupewa sifa mbyaya.
3. Sifa hii ‘eusi’, yaleta wasiwasi.
4. Rangi hii hakika, ni wapi ilitoka?
5. Ibada za Weusi, harusi kuzitusi.
6. Kama mtu mweusi, Lusifa ni mweusi
7. Ibada ya Weupe, hupokewa peupe
8. Adamu naye Hawa, weupe walipewa
9. Yesu Mwana wa Mungu, alikuwa Mzungu
10. Malaika wa Mungu daima ni Wazungu
11. Mweusi ti hatendi, silaumiwe pindi
12. Mweusi duniani, likosa kitu gani?
13. Mweusi jilaumu, measi yako damu.
14. Mweusi umeiga, hata ya kutoiga
15. Asojali mkuu, atavunjika guu
16. Baa mejikatia, nani takulilia?
MASWALI:
(a) Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu yako. (alama 2)
(b) Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
(c) Toa mifano miwili ya matumizi ya mbinu ya inkisari katika shairi hili na uyaandike katika
(d) Eleza maudhui ya shairi hili. (alama 2)
(e) Ni nini dhamira ya mtungaji wa shairi hili? (alama 2) (f) Kwa kutoa m