Download All Documents- (Ksh 299) Full Day
Hurry during this Offer

Study Guide To ‘Bembea ya Maisha’by John W. Wanjala-Mtiririko wa Maonyesho

Read also Study Guide to Riwaya ya ‘Nguu za Jadi’

Mtiririko wa Maonyesho Katika Bembea ya Maisha

SEHEMU I   

Onyesho I   

Nyumbani kwa Sara, Sara ameketi kwenye kochi baada ya kumeza vidonge vya  dawa kwa sababu ya maradhi yanayomsumbua. Yona anayeonekana mchovu na  mwenye kukinai anaingia kwa nyumba.  

Onyesho linaanza kwa kuonyeshwa namna Yona asivyofurahia hali katika  nyumba yake. Analalamikia Sara kuwa hajamwandalia chakula. Yona  hababaishwi na hali ya Sara ya ugonjwa, haja yake ni chumba kivuke moshi. Sara anamweleza namna mwili wake ulivyo, hapo mazungumzo kuhusu mwana wao,  Neema, yanaanza. Yona anatoa wazo lake kwa Sara amwite bintiye aje ampeleke  hospitalini. Sara anakataa wazo hilo kwa kukiri kuwa bintiye ana familia yake  ambayo anafaa kuishughulikia.  

Maoni ya Sara yanazua mgogoro baina yake na Yona kuhusiana na mtoto wao  Neema. Yona anashikilia kuwa ni jukumu la bintiye kuwajibikia matibabu ya  mamake, naye Sara anashikilia kuwa bintiye ana majukumu ya kwake na tayari  amewafanyia mengi, kwa hivyo, awachwe apumzike.   

Mgogoro huu unasawazishwa onyesho linapoelekea kuisha. Sara na Yona  wanakubaliana kuwa wanafaa kumpa binti yao baraka zao.  

Onyesho linamalizika kwa kuonyeshwa Yona akirejelea suala la chakula. Sara  anamweleza asubiri kwa kuwa amempelekea Dina salamu aje awafanyie  chochote.  

MASUALA MAKUU

Onyesho hili linakunjua jamvi la mjadala kuhusiana na majukumu ya watoto kwa wazazi wao. Inabainika kuwa katika jamii nyingi watoto wa kiume ndio  wanaotarajiwa kuwatunza wazazi wanapozeeka.  

Inachukuliwa kuwa watoto wa kike walioolewa wanapaswa kupewa fursa ya  kushugulikia jamii za kule walikoolewa. Ingawa Neema ni mtoto wa kike,  anaonekana kuyamudu majukumu yake kama ambavyo mtoto wa kiume  angaliweza kuyamudu. Msemo wa ‘kutoa ni moyo usambe ni utajiri’  unadhihirishwa na matendo ya Neema. Mazungumzo baina ya Sara na

Yona  yanadhihirisha kuwa hata ajira za kiwango cha chini kama zile za kufanya kazi  shambani na nyumbani pia huwa na changamoto zake. Baadhi ya waajiriwa  huwaibia waajiri wao huku wengine wakidhihirisha hali za uvivu na kushindwa  kutekeleza wajibu wao kama inavyotarajiwa.  

Study Guide To ‘Bembea ya Maisha’-Mtiririko wa Maonyesho

ONYESHO II

  • Onyesho hili linatukia nyumbani kwa Dina. Kiwa alikuwa amefika nyumbani  kumjulia hali mama yake.  
  • Onyesho hili linaanza kwa kuonyeshwa namna Kiwa anavyogusagusa chakula na kudai ametosheka. Katika harakati ya mazungumzo juu ya chakula, Dina na Siwa  wanajikuta wakizungumza kuhusu familia ya Yona na Sara. Dina anamweleza  mwanawe Kiwa namna familia hiyo ilivyodunishwa na wanajamii kwa kukaa  muda mrefu bila kujaliwa na watoto na hata baada ya kufanikiwa na watoto  wasichana, jamii iliendelea kuwasuta na kuwakejeli kwa kuwa hawakujaliwa na  mtoto wa kiume atakayerithi fimbo ya baba yake. Kusemwa huku na wanajamii  kunasababisha Yona kuingia katika ulevi, ulevi ambao unamsukuma kumdharau  na kumchapa bibi yake kichapo cha mbwa.  
  • Onyesho linaisha kwa kuonyeshwa Dina akimuaga Kiwa ili aweze kwenda  kumsaidia Sara katika harakati ya mapishi kwa kuwa Sara alikuwa anaugua.  

MASUALA MAKUU

Onyesho hili linamulika masuala matatu muhimu. Taasubi ya kiume na mila  potovu, ukosefu wa ufahamu kuhusu chanzo cha jinsia ya watoto na umuhimu  wa bidii maishani. Kulingana na somo la Biolojia, chembechembe za kromosomu zinazofanya uamuzi wa jinsia ya mtoto hutokana na wazazi wa kiume ambao  wamebeba kromosomu aina ya Y isababishayo kuzaliwa kwa mtoto wa kiume.  Mwanamke hana uamuzi kuhusiana na jambo hili. Hali ya kuwafedhehesha na  kuwanyanyasa wanawake kutokana na kuzaliwa kwa watoto wa kiume halina  msingi wowote. Tatizo hili linatokana na ubabe dume na taasubi ya kiume. Hali  hii inatiliwa mbolea na utamaduni potovu wa jamii kutaka kumrithisha mtoto  wa kiume na kumkandamiza mtoto wa kike. Suala la bidii maishani linajitokeza  kama kiungo muhimu cha ujenzi wa maisha.  

Dina anajitolea kuwasaidia Sara na Yona katika kazi za nyumbani kutokana na  hali mbaya ya afya ya rafikiye Sara. Tendo hili linadhihirisha udugu na ujirani  mwema.  

ONYESHO III

Onyesho hili linatokea nyumbani kwa Sara, jikoni. Dina yupo katika harakati ya  mapishi naye

Sara amejikunyata kwenye kibao. Mchuzi u tayari. Sara  anamshukuru Dina kwa kufika kumsaidia. Dina anapokea shukrani na kumpa  Sara maneno ya kumtia nguvu. Dina anamweleza Sara kuwa kila kitu hufanyika kwa mpango wa Manani. Anamweleza atazame faraja ilivyovuka kwake kwa vile  watoto wake wamefaulu maishani. Anampa matumaini kwamba atapona kwa  kuwa hospitali ambayo Neema anampeleka ina watalaamu.  

Mazungumzo ya matumaini yanaendelea kunoga huku Dina akiendelea na  mapishi. Dina anauliza Sara alikokwenda Yona na hapo mazungumzo kuhusu  mwanamume na utamaduni yanazuka.  

Tunaelezwa namna utamadumi ulivyowajenga wanaume kama watu wasiofaa  kuingia jikoni.  

Onyesho hili linatimia Sara akimweleza Dina kuhusu mipango iliyopangwa na  Neema kuhusu namna atakavyorudi kliniki kupata matibabu.  

MASUALA MAKUU

Katika onyesho hili inadhihirika wazi kwamba taasubi ya kiume imemtawala  Yona na kumfanya kutoona hali ya unyonge wa mkewe.  

Study Guide To ‘Bembea ya Maisha’-Mtiririko wa Maonyesho

Inamlazimu Sara kuomba usaidizi kwa jirani ndipo waandaliwe chakula ilhali ni  kazi ambayo Yona angeifanya bila malalamishi na kuficha siri ya familia yake.  Suala la wanaume kutosaidia katika shughuli za nyumbani hutokana na mila na  desturi ambazo zinamdhalilisha mwanamke. Mwanamume anapomsaidia  mkewe jikoni huona ni kama kwamba hadhi yake imeshushwa.  

La kutia moyo ni kwamba, ingawa jamii inamdhalilisha mwanamke, ni dhahiri  kuwa mwanamke wa sasa amejizatiti na kujiinua na kufikia kiwango cha  kutajika. Neema anakuwa mfano mzuri katika jamii kwa kuyabeba majukumu  yake binafsi na yale ya nyumbani alikotoka.  

Anahakikisha mama yake anatibiwa na kumfanya Yona amuonee fahari si tu  kama msaidizi bali nguzo muhimu ya kutegemewa hata ingawa ni mtoto wa  kike, tena aliyeolewa.  

Umuhimu wa ujirani mwema pia unazungumziwa. Dina anajitokeza kuwa jirani  na rafiki wa kutegemewa wa Sara. Ni wazi kuwa Sara na Yona wanaishi vizuri na majirani wao.  

SEHEMU II

ONYESHO I

Nyumbani kwa Neema, Neema na mamake wameketi ukumbini wanazungumza.  Sara amefika mjini kwa ajili ya matibabu na amechoka kutokana na safari ndefu.  ⮚ Neema anashangazwa na kuchelewa kwa Lemi kutoka shuleni. Anakumbushwa  na Bela kuwa Lemi anajiandaa kwa hafla itakayofanyika shuleni na ambayo  Neema ameisahau kwa sababu ya  

Neema anamsaili mamake kuhusu sababu za vurumai za mara kwa mara za  Yona. Sara anamweleza kuwa vurumai hizo zilizomsababishia maradhi ya moyo  zilitokana na ulevi; kwamba Yona alitaka amzalie mtoto wa kiume. Jamii nayo  ilimsukuma Yona aoe mke mwingine ili azaliwe mtoto wa kiume ambaye Sara  hakufanikiwa kupata. Yona aliposhindwa kuhimili shinikizo hizo aliingia katika ulevi hadi akafutwa kazi. Mbali na haya, Sara anamtetea Yona kwa hali na mali  kuhusu tabia yake ya ulevi na vurumai.  

Ni katika onyesho hili tunapomwona Neema akilalamika kuhusu Bunju,  mumewe. Kulingana na Neema, Bunju anaonekana mgumu wa pesa. Anajitetea  kwamba amebanwa na mahitaji mengi ambayo hayamwachi na fedha za ziada.  ⮚ Tathmini  

Kupitia kwa mazungumzo haya, masuala kadhaa yanajitokeza yakiwemo  maeneo ya mashambani yaliyopuuzwa kimaendeleo, bidii maishani, taasubi ya  kiume pamoja na athari za uraibu wa pombe. Usemi ‘mrina haogopi nyuki,'(uk.  18) unaotumiwa na Sara unaelezea bidii inayohitajika ili mtu afaulu maishani.  Kwamba, sharti mtu akabiliane na magumu anayokumbana nayo. Sara  anayasema haya anapogundua kuwa Lemi ana kazi nyingi za kufanya huko  shuleni.

Kwa sababu ya kazi hizo, inakuwa vigumu kwa Sara kuonana na mjukuu wake.  

Suala la uwajibikaji miongoni mwa wanasiasa linajitokeza pia. Suala hili  linaangaziwa kupitia usafiri unavyotatizwa na miundo misingi duni katika  sehemu za vijijini.  

Inabainikakwambayonaanajitokomezaulevinikutokananamsukumo wa  wanajamii kwa kukosa kuzaa mtoto wa kiume. Huu ni utamaduni uliopitwa na  wakati. Pombe inakuwa kimbilio la kumsahaulisha malengo aliyoshindwa  kuyafikia. Sara anasisitiza kwamba wazazi wana wajibu wa kumlea mtoto wa  jinsia yoyote ile bila ubaguzi.  

Study Guide To ‘Bembea ya Maisha’-Mtiririko wa Maonyesho

ONYESHO II

Onyesho hili linafanyika nyumbani kwa Neema akiwa na Bela, mfanyakazi wake.  Kupitia mazungumzo yao inabainika kwamba maisha ya leo yana changamoto  nyingi kiasi kwamba wazazi hawatangamani na watoto wao jinsi  

inavyotakikana. Hali hii inaonekana kuwakera wazazi.  

🙓 Suala la shughuli nyingi kazini linaonekana kuhitilafiana na shughuli ya malezi.  Katika sehemu hii inabainika kuwa Neema haonani na Lemi kwa sababu kila  afikapo nyumbani mtoto huwa amelala.  

🙓 Suala la mila pia linaibuka. Wazazi wa Sara hawawezi kulala kwa mtoto wao  aliyeolewa. Neema analizungumzia jambo hili kwa mshangao. Hili ni jambo la  kutatiza kwa sababu mara kwa mara mamake Neema huenda mjini kwa  shughuli za matibabu na huwa anahitaji mahali pa kulala.  

🙓 Isingekuwa kwamba Asna anaishi mjini na kwamba anaweza kumuauni  mamake, basi ingempasa Neema kumkodishia chumba mamake, jambo ambalo  Kiafrika ni makosa. Suala la utandawazi linajitokeza na ni dhahiri kwamba  baadhi ya mila zimepitwa na wakati na zinapaswa kutupiliwa mbali kama Bela  anavyoeleza:  

🙓 Hayo ni ya kale…na ya kale hayanuki. Wengi hawafuati tena mila hizo.  Walimwengu sasa wanavaa sare moja (uk. 24). Kauli hii inaonyesha namna mabadiliko ya kijamii yamefanya baadhi ya mielekeo ya kitamaduni kupuuziliwa mbali.  

Masuala makuu

Sehemu hii inadhihirisha jinsi hali za maisha ya kisasa zinavyowatatiza wanajamii.  Wanalazimika kufanya kazi mchana kutwa ili kujikimu na kuzifaa familia zao. Matokeo  ni kwamba hawapati nafasi ya kutangamana na familia zao ipasavyo. Ni bayana  kwamba bado wanajamii wamefungwa na mila ambazo kwa hakika ni vigumu kuzitii  kwa sababu ya maisha ya kisasa. Mfano mzuri ni miko inayowazuia wakwe kutolala  katika makaazi ya wana wakwe zao.  

Onyesho Ill

Katika onyesho hili Bunju yuko tayari kuondoka kwenda kazini asubuhi.  Mazungumzo na mkewe Neema yanahusu matokeo ya mitihani ya Lemi, mtoto  wao. Huku Neema akionekana kuridhishwa na matokeo hayo Bunju anamtaka  Lemi kujitahidi zaidi ili apate matokeo ya kuridhisha zaidi. Mgogoro baina ya  wazazi kuhusu masomo ya watoto wao unajitokeza. Hali ya Neema na Bunju  kutokubaliana kuhusu bidii ya mtoto wao inaweza kuzua msukosuko.  

Neema anapomwelezea Bunju kuwa mamake tayari ameshafika mjini kwa  matibabu, anakataa kutoa pesa za kusaidia matibabu hayo. Bunju anadai kuwa  ana majukumu mengi. Kwamba anagharamia mahitaji yote ya nyumbani,  yakiwemo karo ya shule, kodi ya nyumba na amemnunulia Neema gari.  Anamtaka Neema awajibike kwa sababu amemruhusu kutumia mshahara wake  kwa mahitaji ya familia yake.  

Bunju anasisitizia ile dhana ya kutomruhusu mama mkwe kulala nyumbani  kwao. Mila na desturi hizo zinamkera Neema sana. Kwa Neema, hizo ni mila na  desturi zilizopitwa na wakati.  

TATHMINI

  • Onyesho hili linazungumzia mambo muhimu ya kifamilia, hasa malezi na elimu.  Neema anaridhishwa na matokeo ya mwanawe, ila Bunju anamtaka Lemi  aongeze bidii masomoni. Hayo yakijiri, inaonekana kana kwamba ni Neema  pekee anayejitahidi kushughulikia matakwa ya Lemi shuleni. Bunju analipa karo  na kutekeleza majukumu mengine ila kazi yake imembana hadi hana muda wa  kutangamana na familia yake ipasavyo. Mfumo wa uchumi umewagandamiza  raia na kuwalazimisha kufanya kazi masaa mengi kupindukia.  
  • Mfumo wa elimu unawapa watoto shinikizo la kujibidiisha zaidi masomoni,  jambo ambalo linaweza kusababisha msukumo wa kiakili miongoni mwa  watoto. Ni bora wazazi wakiwa na msimamo mmoja kuhusu masuala  yanayohusu elimu ya watoto wao.  
  • Mchango wa mwanamke katika ndoa unamulikwa. Bunju analipa kodi ya  nyumba, karo na hata kamnunulia mkewe gari. Je, mchango wa mkewe katika  

majukumu ya kifamilia ni upi? Ni muhimu mwanamke anayefanya kazi  kuwekeza kiwango fulani cha pato lake katika mali ya familia ili kupata heshima  na pia kama njia mojawapo ya kujifunza kuimudu familia ikiwa ataondokewa na  mumewe mapema.  

ONYESHO IV

Mjini, nyumbani kwa Asna. Asna anamwandalia mamake kiamshakinywa. Mama  mtu anashangaa mbona bintiye anaishi katika chumba kidogo. Bintiye anajitetea  kuwa chumba hicho kiko katika mtaa wa kifahari na anakifurahia. Sara  analinganisha maisha ya mjini na ya kijijini na kuona kuwa yale ya mjini yanaudhi,  afadhali ya kijijini.  

Anasema kwamba, watu wa mjini wako mbioni kila wakati na mapato yao ni haba.  Asna hakubaliani na mamake; kwake, kiwango chake cha elimu hakimruhusu  kwenda kukaa kijijini.   🕮 Sara anamsihi Asna aolewe amletee mjukuu. Asna hakubaliani na jambo hilo.  Kulingana na Asna, ndoa ina matatizo mengi kama yale anayopitia Neema, dada  yake, ambaye ingawa amesoma na kupata shahada mbili, hazimsaidii kupigana na  msimamo wa kitamaduni alionao Bunju, mumewe. Badala ya kupigania mabadiliko  ya msimamo wa Bunju, Neema anaonekana kuukubali kwa sababu ya uhuru wa  matumizi ya mshahara wake aliopewa na Bunju.  

Utepetevu kazini unazungumziwa kupitia madaktari na utendakazi wao. Baadhi ya  madaktari daima wako mbioni kutoka hospitali moja hadi nyingine ili kuchuma hela za ziada bila kuwazingatia wagonjwa wao kikamilifu.  

MASUALA MAKUU

Kuna mambo muhimu yanayojadiliwa katika onyesho hili. Jambo la kwanza ni  hadhi. Ile hali ya kutaka kuishi sehemu za kifahari hata ingawa pato ni dogo.  Asna anaishi maeneo ya juu ingawa mazingira ya nyumba yake ni duni.  Anajikakamua kulipa kodi ya juu ya nyumba bila kujali mazingira anamoishi.  

Jambo la pili linaakisi athari za elimu ya juu dhidi ya mila na desturi za Kiafrika.  Inasahaulika kwamba,elimu pekee bila uelewa haiwezi kubadilisha dhana na  fikra za kitamaduni. Bunju ana elimu lakini elimu yake haijamtoa katika mila na  desturi za jamii yake. Neema ana elimu lakini haimsaidii kuelewa chanzo cha  mila na desturi za Bunju. Jambo la tatu ni kutosheka kwa mwanamke. Neema  anaonekana kutosheka na hali ya mumewe ya kumruhusu kutumia pesa zake  atakavyo. Hafikirii kuwa huenda ikawa ni mtego. Mara nyingi mwanamke  anapopata uhuru wa aina hii, huweza kubugikwa na akili asiweze kufikiria  kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadaye. Kisha mambo yanapoharibika  hujikuta hana lolote la kutegemea. 

Study Guide To ‘Bembea ya Maisha’-Mtiririko wa Maonyesho 

Sehemu III

ONYESHO I

Nyumbani kwa Neema na Bunju. Neema yuko nyumbani anafanya usafi.  Anafikiria jinsi ugonjwa wa mamake ulivyomfanya fukara. Bunju anapoingia  chumbani, Neema hamsikii, anashtuka. Kwa mara nyingine, anakataa kumsaidia  Neema kugharamia ugonjwa wa mamake.   🙓 Anasema kwamba anafanya majukumu yote ya pale nyumbani na haoni ni kwa  nini Neema hawezi kuupangia mshahara wake ili uweze  

kuyakidhi mahitaji yake. Neema anahuzunishwa na msimano wa Bunju lakini pia anakumbuka maneno ya mamake kuwa Bunju ni zawadi kwake, jambo ambalo  linampa heri kidogo.  

Masula makuu

Onyesho hili linampa msomaji au mtazamaji nafasi ya kuelewa mahusiano katika taasisi ya ndoa. Wanandoa hao wawili wanashikana mkono kuendeleza maslahi  ya jamii yao. Mume anaheshimu rai ya mkewe ya kutumia hela zake  kushughulikia wazazi wake ambao ni wahitaji.  

Mama ni mgonjwa na baba yake amepoteza ajira. Tofauti ya matumizi ya pesa  kati ya mwanamke na mwanamume yanajitokeza. Mwanamume anajenga na  mwanamke anapamba. Mambo yanapoharibika, mwanamke huachwa bila  makao kwa sababu ya dhana kuwa hakuwekeza katika  

ujenzi wa nyumba. Hili ni jambo linalohitaji mjadala zaidi. Bunju anajitokeza  kama mwanamume anayefanya majukumu yote ya kifamilia, hali ambayo  haimtayarishi mkewe kwa maisha ya baadaye iwapo mambo Kuna pia suala la  matumizi ya pesa ili kutibu magonjwa. Familia nyingi yataharibika. hazina bima  ya matibabu. Magonjwa yanapobisha hodi basi huziacha baadhi ya familia hizo  katika hali ya umaskini. Wengi huitisha michango kama Neema anavyoitisha  msaada kutoka kwa Bunju.  

Katika mazungumzo yao, pia inadhihirika wazi kwamba mapato ya kazi moja  hayatoshi kamwe.

Umuhimu wa kujishughulisha zaidi ili kuweza kuyamudu  mahitaji unajitokeza.  

ONYESHO II

Sara yuko hospitalini ambako amelazwa. Neema na Asna wamefika kumwona.  Sara anataka kuruhusiwa kwenda nyumbani kwa sababu gharama ya hospitali  inaendelea kupanda. Sara analinganisha huduma za matibabu za kule kijijini na  za mjini. Hospitali za mjini ni kama hoteli ilhali za kijijini ni kama seli ambako  mtu akilazwa hata matumaini ya kupona hudidimia.  

Sara anataka atoke hospitalini arudi kijijini kwenda kumsaidia Yona ambaye  alimwachia kazi zote za nyumbani. Bunju anafanya shughuli zake bila kupita  hospitalini kumjulia hali Sara. Jambo hili linamkera Asna ambaye anamwona  Bunju kama mchoyo na asiyewajibika kuhusu mkwe wake. Neema anamtetea  Bunju.  

Anasema kwamba tabia yake inatokana na jinsi alivyolelewa, kwa hivyo  wasimlaumu.  

Study Guide To ‘Bembea ya Maisha’-Mtiririko wa Maonyesho

MASUALA MAKUU

Mazungumzo haya yanaibua mambo matatu muhimu kuhusu hospitali  aliyopélekwa Sara. Mosi, malazi na chakula ni vya hali ya juu. Pili, gharama ya  huduma ni ya juu mno. Tatu, hospitali hiyo ina aina nyingi za wataalamu. Hali hii inakinzana na hali ilivyo katika baadhi ya hospitali nchini ambazo ni duni na  hutoa huduma mbovu zinazomfanya mgonjwa kutamauka na kukata tamaa.  

Hospitali za kibinafsi hutoa mazingira mema zaidi ya kimatibabu na ni mwafaka  zaidi kwa wale wanaoweza kulipia gharama zake, Mazingira ya hospitali za  umma ni duni, nyingi zikiwa hazina huduma bora, hazina madaktari na hata  dawa za kutosha.  

Pia, mwanamume angali anapewa hadhi ya juu kuliko mwanamke. Jamii  haimruhusu mwanamume kufanya kazi za jikoni kwa sababu kazi hizo  huchukuliwa kuwa ni za kike. Ndiposa, ingawa Sara angali mgonjwa, bado ana  ari ya kurudi nyumbani kumshughulikia Yona, mumewe.  

Bunju amechorwa kama mtu asiyemjali mama mkwe. Ingawa Neema  haridhishwi na hali hiyo, anashindwa kumkabili na kusingizia malezi. 

Heshima anayopewa mwanamume na mwanamke katika onyesho hili,  inawekwa kwenye mizani.  

Study Guide To ‘Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine’

1 thought on “Study Guide To ‘Bembea ya Maisha’by John W. Wanjala-Mtiririko wa Maonyesho”

Leave a Comment