MASWALI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Zitavuma,
Zitakoma,
Nitakwima, Mti-mle.
Na muda nikisimama,
Nitatongoa nudhuma, Kwa tenzi zilizo njema, Nilisifu mti – mle.
Tazipanga tathlitha, tungo zilizo na hekima, Za huba na thiatha, za kuburudi mitima, Mashairi mabuthutha, musome mnaosoma.
Mti nishainukia,namea kuwa mzima,
Mizizi yadidimia, ardhini imeuma, Nanena kitarbia, tungo zilizo adhama Japo ni tungo za zama, mti-mle hutumia.
Zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,
Dharuba kinitikisa, mti-mle huinama,
Huyumba nikaziasa, matawi yakakingama,
Gharika ikishapisa, hurudi nikawa wima, Na tungo za takhimisa, mti-mle huzipima.
Maswali
- Shairi hili ni la kimapokeo. Toa sababu mbili kuunga kauli hii. (Alama.2)
- Taja bahari kuu ya ushairi ambayo imetumiwa na mshairi. Fafanua. (Alama.2) (c) Fafanua dhamira ya mshairi. (Alama.2)
- Kwa kutoa mifano bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili.
(Alama.2)
- Eleza jinsi mshairi ametumia idhini ya ushairi katika utungo huu. (Alama.2)
- Andika ubeti wa nne kwa lugha natharia. (Alama.4)
- Mshairi anamaanisha nini anaposema ‗zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,‘(Al2)
- Eleza toni ya shairi hili. (Alama.2)
- Eleza maana ya msamiati ufuatao.
- Nitatongoa
- Zitapusa. (Alama.2)
KCSE USHAIRI 2
MASWALI
USHAIRI.
Soma shairi hili kisha ujibu maswali.
Sinusubuwe akili, nakusihi e mwandani
Afiya yangu dhahili, mno nataka amani
Nawe umenikabili, nenende sipitalini Sisi tokea azali, twende zetu mizimuni Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
Mababu hawakujali, wajihisipo tabani
Tuna dawa za asili, hupati sipitalini
Kwa nguvu ya kirijali, mkuyati uamini Kaafuri pia kali, dawa ya ndwele fulani Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani.
Mtu akiwa halali, tumbo lina walakini
Dawa yake ni subili, au zogo huauni
Zabadi pia sahali, kwa maradhi yalo ndani Au kwenda wasaili, wenyewe walo pangani
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani
Mtu kwenda sipitali, nikutojuwa yakini.
Daktari kona mwili, tanena kansa tumboni
Visu vitiwe makali, tayari kwa pirisheni Ukatwe kama figili, tumbo nyangwe na maini
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani
Japo maradhi dhahili, kuteguliwa tegoni,
Yakifika sipitali, huwa hayana kifani
Waambiwa damu, kalili ndugu msaidieni
Watu wakitamali, kumbe ndio buriani
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani
Mizimu wakupa kweli, wakueleze undani
Maradhiyo ni ajali, yataka vitu dhamani
Ulete kuku wawili, wamajano na wa kijani Matunda pia asali, vitu vyae chanoni Nifwateni sipitali, na dawa zi mlangoni?
MASWALI.
- Lipe shairi hii anwani mwafaka. (al.1)
- Toa sababu zinazofanya mshairi kutokana kwenda hospitali. (al.3)
- Andika ubeti wanne kwa lugha ya nathari/ tutumbi. (al.4)
- Taja bahari mbili zilizotumika katika shairi hili. (al.2)
- Tambua nafsineni katika shairi hili. (al.1)
- Tambua toni ya shairi hili. (al.1)
- Eleza muundo wa shairi hili. (al.4)
- Fafanua uhuru wa mshairi unavyojitokeza katika shairi hili. (al.2)
- Andika maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi hili.
(al.2)
(i)Dhalili
(ii) Azali
KCSE USHAIRI 3
MASWALI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. (alama 20) Barabara.
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nitulize akili
Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruba Sasa naona unyoofu wake Unyoofu ambao unatisha zaidi.
Punde natumbukia katika shimo
Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena,
Ghafla nakumbuka ilivyosema Ile sauti zamani kidogo
“Kuwa tayari kupanda na kushuka”.
Ingawa nimechoka
Jambo moja li dhahiri
Lazima niifuate barabara
Ingawa machweo yaingia
Nizame na kuibuka
Nipande na kushuka
Jambo moja nakumbuka: Mungu Je, nimwombe tena? Hadi lini? Labda amechoshwa na ombaomba zangu Nashangaa tena!
Kitu kimoja nakiamini
Lazima niendeleee kujitahidi kw akila hatua mpya
Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
Nikinaswa na kujinasua,
Yumkini nitafika mwisho wake
Ikiwa wangu mwisho haitauwahi kabla.
(Timothy Arege)
Maswali:
- Taja na ueleze aina ya shairi hili. (alama 2)
- Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
- Fafanua dhamira ya shairi hili. (alama 2)
- Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili. (alama 3)
- Tanakali za sauti
- mbinu rejeshi
- Taswira
- Eleza umuhimu wa maswali balagha katika shairi. (alama 2)
- Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari. (alama 4)
- Eleza matumizi ya mistari mishata katika shairi hili. (alama 2)
- Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumika katika shairi. (alama 3)
- Kuruba
- siha
- machweo
KCSE USHAIRI 4
MASWALI
Soma shairi hili kisha ujibu maswali
- Punda kalibebe gari, gari limebeba punda Mwalimu ana pakari, muashi vyuma adunda Jaji gonga msumari, sonara osha vidonda.
Kinyume mbele
- Saramala ahubiri, muhunzi tiba apenda
Mganga anaabiri, baharini anakwenda
Hata fundi wa magari, anatomea vibanda
Kinyume mbele
- Wakili anahiyari, biashara kuitenda Mtazame askari, akazakaza kitanda,
Mkulima mashuhuri, jembe limemshinda
Kinyume mbele
- Apakasa daktari, ukili anaupinda
Saveya kawa jabari, mawe anafundafunda,
Hazini wa utajiri, mali yote aiponda,
Kinyume mbele
- Msemi huwa hasemi, wa inda hafanyi inda
Fahali hawasimami, wanene waliishakonda
Walojitia utemi, maisha yamewavunda
Kinyume mbele
- Kiwapi cha kukadiri, twavuna shinda kwa shinda
Tele haitakadari, huvia tulivyopanda
Mipango imehajiri, la kunyooka hupinda Kinyume mbele
MASWALI
- Mtunzi alikuwa na malengo gani alipotunga shairi hili? (alama 3)
- Licha ya tarbia, eleza bahari nyingine zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 4)
- Eleza namna mtunzi alivyoutumia uhuru wake. (alama 5)
- Ni mbinu gani inayotawala shairi hili? (alama 2)
- Uandike ubeti wa nne katika lugha nathari. (alama 4)
- Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
KCSE USHAIRI 5
MASWALI
Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali
Ulimwengu ulimwengu, ulimwengu naratibu
Yaliyo kichwani mwangu, nataka kuyatubu Wayasome ndu zangu, wa mbali na wa karibu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ulimwengu ni kiwanja, cha wenye raha na tabu
Wengine wanajikonja, kwa wengine ni adhabu Kucha na kutwa twahanja, kutafuta matulubu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa balaa, aliniusia babu
Mna mambo yamejaa, ya faraja na kusibu Na machache ya kufaa, ila mengi ya udubu Cha wenye raha na tabu,ulimwengu ni kiwanja.
Ni kiwanja cha Amina,Saidi Ali Rajabu
Wengine kitu hatuna, tunaishia kababu Wale wamejaza sana, wanashindwa kuhesabu Cha wenye raha na tabu, Ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa urongo, na kweli pia ajabu
Kichwa hudanganya shingo, tumbo kiuno chasibu Usitumai ubongo, wa nduguyo na swahibu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa walevi, pombe kwao ni dhahabu
Mara vile mara hivi, wakilewa majudhubu Maneno ya kiujuvi, hujipaka hata shabu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni kiwanja wenye dini, wamtiio wahabu
Mashekhe msikitini, humo humfanya muhibu
Mapadiri kanisani, huvihubiri vitabu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa malofa, lofa mtu mwenye tabu
Kusema sana kashifa na moyo kisebusebu Tunakaribia kuja, kwa kushindwa kujimudu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa faraja, alowajali habibu
Na wengine sitotaja, msinambe ninagubu Ni uwanja wa viroja, vigumu kuvikutubu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Maswali
(a)Lipe shairi hili anwani ifaayo. (alama 1)
(b) kwa kutoa mfano, eleza mbinu zozote mbili za lugha zilizotumika katika shairi.
(alama 2)
(c)Eleza jinsi uhuru wa mshairi ulivyotumika katika shairi. (alama 2)
(d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi. (alama 4)
(e)Taja na ueleze bahari zozote mbili zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
(f)Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
(g)Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
(h)Fafanua dhamira ya mshairi. (alama 2) (i)Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi. (alama 2) (i) Malofa:
(ii) Udubu: