Nguu Za Jadi Questions And Answers-KCSE
contact 0754238886 for answers
QUESTION 1
Fafanua namna ukiukaji wa haki umeendelezwa katika hadithi zifuatazo (alama 20)
a) Fadhila za Punda
b) Sabina
c) Kifo cha Suluhu
d) Nipe Nafasi
QUESTION 2
2 a. “Pupa imenitumbukiza kwenye kisima nilichochimba, sasa naingia mwenyewe …”
a) Bainisha mbinu za kimtindo katika dondoo hili. (alama 2)
b) Huku ukitolea mifano mwafaka, onyesha ukweli wa kauli hii. (alama 8)
Kila Mchezea Wembe: Pauline Kea Kyovi
2b. “Dunia hii nayo kubwa, anasa zake nyingi huwezi kuzimaliza”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Fafanua toni katika dondoo hili. (alama 2)
c) Jadili namna ambavyo anasa imejitokeza katika hadithi hii. (alama 4)
QUESTION 3
2. Ahadi ni Deni-Rayya Timammy
a. `Maudhui ni kipengele muhimu katika kazi ya kisanii.’ Thibitisha dai hili kwa kurejelea
maudhui yafuatayo katika hadithi,Ahadi ni Deni. Alama 10
i. Uwajibikaji
ii. Nafasi ya wanawake
b. “ Ni vigumu kwa binadamu kuungama jambo kama hili ila kwa sasa naona ndiyo njia ya
pekee ya kuinusuru nafsi yangu.’’
i. Weka maneno haya katika muktadha. Alama 4
ii. Wahusika wengi katika hadithi Toba ya Kalia ni wasaliti. Eleza kikamilifu.
Alama 6
Au
3. Kila Mchezea Wembe
“Watu wanaomboleza nikaja na fujo zangu bila kujali wala kubali na kuvuruga shughuli
maziarani.’’
a. Eleza muktadha wa maneno haya. Alama 4
b. Tathmini athari kumi na mbili za unywaji pombe kwa kurejela hadithi hii.
Alama 12
c. Kwa kutoa hoja nne hadithini, eleza umuhimu wa mnenaji. Alama 4
QUESTION 4
(a) Mzimu wa kipwerere-Yussuf Shoka
“Siku iliyofuata, majira ya magharibi pevu, nilifika pale mzimuni. Kama ilivyo ada yangu,
nilivaa guo jeupe lililonifunika gubigubi kama maiti. nikaangalia huku na huko, sikuona mtu.
Hapo nikasogea karibu zaidi na ule mzimu. Nilipofika nikauimba ule wimbo wote.
Nilipomaliza tu nikajitoma kichakani mle bila hofu wala kimeme…nilichokiona humo,
sikuamini macho yangu! Mle ndani ya mzimu mlikuwa na makanda na makasha ya
tumbaku, unga wa kilevi na bangi kwenye marobota. Kulikuwa na mapipa ya chang'aa na
tembo ya mnazi. Humo pia, mlikuwa na kitanda cha besera kilichotandikwa vizuri. Juu ya
kitanda hicho, palitupiwatupiwa asumini na maua ya mlangilangi..”
a)Eleza aina nne za taswira katika kifungu hiki. (al 4)
b)Ukirejelea hadithi ya" Mzimu wa Kipwerere," Fafanua jinsi imani katika mambo ya
kichawi yamejikita katika jamii. (al 6)
(b)Mapambazuko ya Machweo – Clara Momanyi
Onyesha vile Jua la Macheo linawabishia wahusika mbalimbali katika Machweo
yao (al 10)
HADITHI FUPI-MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI
NYINGINE
“Kwa nini nisilipe ?Mnadhani mashaibu kama sisi ni mafukara hohehahe hatuna pesa
mfukoni ?Hebu twende naona dereva yule ana haraka sana.Mkimbize!”
a) Tambua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Onyesha mbinu za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
c) Msemaji wa dondoo hili ana sifa gani? (alama 6)
d) Migogoro tofauti tofauti imeshuhudiwa katika hadithi hii .Thibitisha. (alama 6)