Find Also Study Guide To ‘Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine’
Maswali
1. ..iwapo penzi hili litatia doa, basi nirudishie mfuko huu kama ishara ya kulitupa penzi langu kama jongoo na mti wake…”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Fafanua mbinu mbili ambazo zimetumika katika dondoo hili.
(alama 4)
c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6)
d) Eleza umuhimu wa msemewa wa hadithi hii katika kujenga ploti.
(alama 6)
2. Kwa kurejelea hadithi zifuatazo, jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii. (alama 20)
i. Toba ya kalia ii. Ahadi ni deni iii.
iii. Nilitamani iv. Pupa
3. Wanaume katika mataifa mengi barani afrika wametawaliwa na ubabedume. Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya “Fadhila za Punda” (al.20)
4. Huku ukitolea mifano mwafaka ,eleza jinsi ambavyo haki za watoto/vijana zimekiukwa katika hadithi ya Mapambazuko ya Machweo (alama 20)
5. Mwandishi katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia alifaulu kutumia mbinu ya uwili. Thibitisha. (al. 20)
6. Mwandishi wa hadithi ya “mapambazuko ya machweo” uwajibikaji kwa kiasi kikubwa mno. Illihirisha ukweli na kauli hii
(alama 20)
MASWALI ya Mapambazuko Ya Machweo
7. Wafanyikazi katika nchi nyingi zinazoendelea wanakumbwa na changamoto nyingi sana. Thibitisha hali hii kwa kurejelea hadithi ya ” harubu ya Maisha
(alama 20)
8. Ukombozi wa wanawake unakumbwa na vizingiti vingi sana. Jadili ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi ya sabina.
(alama 20)
9. Fafanua changamoto wanazokumbana nazo waajiriwa katika hadithi Harubu ya Maisha (alama 20)
10. NDOA ni taasisi iliyokuzwa katika hadithi fadhila za punda. Fafanua alama 20
11. “mwanangu, nizike duniani unifunike…”
i) Fafanua muktadha wa maneno haya. (al.4)
ii) Taja na utolee mfano mbinu moja ya kimtindo inayojitokeza katika dondoo hili (al.2)
iii) Ukirejelea hadithi ya” Mzimu wa Kipwerere,” Fafanua jinsi imani katika mambo ya kichawi yamejikita katika jamii. (al.14)
12. Fafanua jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika hadithi ya Nipe nafasi
alama 20
13. “Thank you. U mteja wa pekee, unajua kuthamini huduma nzuri unapopewa.”
i) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (al.4)
ii) Taja na ueleze mbinu mbili za kimtindo katika dondoo hili.(al.4)
iii) Kwa kurejelea hadithi ya “Kila Mchezea Wembe,” Fafanua changamoto zinazowakumba watumiaji wa vileo kupita kiasi. (al. 12)
14. “…iwapo penzi hili litatia doa, basi nirudishie mfuko huu kama ishara ya kulitupa penzi langu kama )ongoo na mti wake…
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Fafanua mbinu mbili ambazo zimetumika katika dondoo hili. (ala 4)
c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6)
d) EIeza umuhimu wa msemewa wa hadithi hii katika kujenga ploti. (al 6)
15. Kwa kurejelea hadithi ya Ahadi ni Deni, fafanua namna Uwajibikaji umejitokeza. (alama 20)
MASWALI ya Mapambazuko Ya Machweo
16. “Kwa kweli, nimeungulika sana miaka yote hii kwa unyama tuliomtendea Jack.. .”
Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
Jadili umuhimu wa msemaji wa dondoo hili. (alama 6)
Jadili ukatili aliokuwa ametendewa mhusika Jack kulingana na dondoo hili. (alama 5)
Kwa kurejelea mhusika Jack, jadili maudhui ya nafasi ya vijana.
(alama 5)
17. Onyesha namna mwandishi wa hadithi ya Nipe Nafasi alivyodokeza maudhui ya taasubi ya kiume.
18. …wajua siku hizi huwezi kuamini yeyote apitaye na hasa akiomba msaada au umekua kututapeli?”
Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
Eleza umuhimu wa msemewa wa maneno haya katika kujenga maudhui
kwenye hadithi hii. (alama 10)
- Eleza sifa za msemaji wa maneneo haya. (alama 5)
19. Kwa kurejelea hadithi zifuatazo, jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii. (alama 20)
Toba ya Kalia
Ahadi ni Deni
Nilitamani PUPA
20. Rachel Wangari katika hadithi ya mapambazuko ametumia mbinu ya JAZANDA kwa upana. Jadili alama 20
21. Swala la Elimu limepewa kipaumbele katika hadithi ya sabina.
Jadili alama 20
22. Fafanua jinsi Yusuf Shoka Hamad katika hadithi MZIMU WA KIPWERERE ameshughulikia swala la ushirikina na unafiki alama 20
MASWALI ya Mapambazuko Ya Machweo
23. Umaskini ni donda sugu katika hadithi kifo cha suluhu, huku ukitoa hoja ishirini jadili alama 20
24. Eleza jinsi ubabedume umejitokeza katika hadithi ya nipe nafasi alama 20
25. Fafanua Changamato Wanazo Kumbana Nazo Waajiriwa Katika Hadithi
Harubu Ya Maisha Alama 20
26. Jadili Matumizi Ya Pombe Haramu Na Athari Zake Katika Hadithi Kila
Mchezea Wembe Alama 20
27. Fafanua wa ufaafu wa anwani Fadhila za Punda (alama 20)
28. NDOA ni taasisi iliyokuzwa katika hadithi fadhila za punda. Fafanua
alama 20
MASWALI ya Mapambazuko Ya Machweo
29. Fafanua Dhiki/Changamoto Zinazowakumba Raia Katika Hadithi Msiba Wa Kujitakia
30. Jadili ufaafu wa anwani Mapambazuko ya Machweo (alama 20)
31. Fafanua dhana ya AJIRA katika hadithi mapambazuko ya machweo
alama 20
32. Urumo umekita mzizi katika jumuiya ya Mapambazuko ya Machweo.
Jadili (alama 20)
33. Miti katika misitu ilizidi kuangamizwa kwa makali ya shoka lakini miti ilizidi kulifurahia shoka…miti ikafikiri shoka ni mmoja wao!”
(alama 20)
- a) Kwa kuzingatia hadithi ya harubu ya maisha, jadili changamoto
zinazokumba asasi ya ndoa. (alama 5)
- Kwa kuzingatia hadithi ya harubu ya maisha, fafanua matatizo
yanayowakumba wafanyikazi. (alama 10)
- Jadili dhana ya utatu inavyojitokeza katika diwani ya mapambazuko ya
machweo na hadithi nyingine. (alama 5)
35. “tafadhali nisamehe…ni barua ilinikawiza…”
- Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 4)
- Tambua kipengele kimoja cha kifani kilichotumiwa katika dondoo hili.
(alama 2)
- Eleza barua hii na matokeo yake. Alama 6)
- Jadili dhima ya msemaji katika kuendeleza maudhui ya hadithi.
(alama 8)
thanks